Home » » WATU 300 KUPATA HUDUMA YA UPASUAJI WA MACHO KATIKA HOSPITAL MPYA ILIYOPO CHUO KIKUU CHA DODOMA YA BENJAMIN MKAPA

WATU 300 KUPATA HUDUMA YA UPASUAJI WA MACHO KATIKA HOSPITAL MPYA ILIYOPO CHUO KIKUU CHA DODOMA YA BENJAMIN MKAPA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa
 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin MkapaHospital Mpya iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka vyuo vya UTAH (Moran aye Centre) na Chuo cha Weil Cornell Medicine vyote vya nchini Marekani wanatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya macho. 


Vifaa vya Kisasa kabisa na madaktari bingwa hawa watakuwepo kuanzia tarehe 22 hadi 25 mwezi huu wa pili 2016.Huduma hizi zinatolewa bure kabisa. Hii ni kutoka na Mahusiano yaliyopo kati ya Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo hivi. 
Watu 300 wanatarajiwa kupata  huduma ya upasuaji kwa kipindi hiki. Katika Mahojiano na Dr. Jeff kutoka Chuo Kikuu cha UTAH (Moran aye Care alisema kuwa wanafanya huduma hizi pia nchi nyingi lakini kwa Dodoma tatizo ni kubwa zaidi. Alieleza kuwa mpango wao kwa sasa ni kuja Dodoma mara mbili kwa mwaka. 
Pia wanasaidia sana katika kuwafundisha madaktari wetu wa kitanzania na hadi sasa Dr. Frank ambaye ni mwalimu katika Chuo cha afya cha Chuo Kikuu cha Dodoma amefaidika na mafunzo hayo na tayari anafundisha madaktari wengine. 
 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa
Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa