Home » » WAZIRI WA FEDHA AENDEKEA KUNG'ANG'ANIWA BUNGENI.

WAZIRI WA FEDHA AENDEKEA KUNG'ANG'ANIWA BUNGENI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
Baada ya serikali kukwama kuwasilisha bungeni mapendekezo ya mwelekeo wa mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21, jana iliwasilisha mwongozo wa kuandaa  mpango wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/17, jambo ambalo lilizua taharuki kwa mara nyingine.
 
Kabla Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, kusoma mwongozo huo, wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, walisimama kuomba mwongozo wa kiti.
 
Kwa upande wake, Lissu alisema kanuni ya 94 (1) inasema katika mkutano wake wa Oktoba na Novemba kila mwaka, Bunge kwa siku zisizopungua tano litakaa kama kamati ya mipango ili kukidhi matakwa ya sheria ibara ya 63(3)(C) ya katiba inayotaka kujadili mpango wa muda mrefu au mfupi na kuutungia sheria.
 
Lissu pia alitumia kanuni ya 97 (1) inasema “Tarehe 11 ya mwezi wa tatu kila mwaka na tarehe nyingine inayofuata ambayo itakuwa sio siku ya kazi, waziri anayehusika na masuala ya mipango atawasilisha kwa wabunge mapendekezo ya serikali ya mpango kwa mwaka,” alisema na kuongeza:
 
katika orodha ya shughuli za leo kuna kitu kimeletwa hapa mapendekezo ya mpango wa taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali katika mwaka wa fedha 2016/17, kanuni ya 94 inasema tupate mapendekezo ya utekelezaji wa mpango sio mapendezo ya mpango ni mapendekezo ya utekelezaji wa mpango na ibara ya 63(3)(c)inasema tupate mpango wenyewe.
 
Mheshimiwa Spika wewe ni mzoefu wa bunge hili, mwaka 2011 tuliletewa mpango wa taifa wa mwaka mmoja na mwaka 2014/15 tuliletewa mpango wa maendeleo ya taifa wa mwaka mmoja leo 2016/17 tumeletewa mapendekezo ya mwelekeo wa mpango wa maendeleo ya Taifa 2016/17.
 
Hichi kitu hakipo kwa mujibu wa katiba ambayo inasema kujadili na kuidhinisha mpango na kuutungia sheria, hichi kitu kinacholetwa hakilingani na kanuni kwasababu kanuni ya 94 inasema utekelezaji wa mpango maana yake lazima kuwe na mpango, tulipaswa tuwe na kitu kama hiki, hii kitu haijawahi kuletwa kwenye bunge hili, haipo kwenye kanuni wala kwenye katiba,” alisema Lissu.
 
CHANZO ; NIPASHE.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa