Home » » ZITO KURUDISHWA PAC, MBATIA BAJETI.

ZITO KURUDISHWA PAC, MBATIA BAJETI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Baada ya malalamiko ya wabunge wa upinzani juu ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kuzipangua kamati hizo.
 
Taarifa ambazo Nipashe imezipata mjini hapa jana, licha ya kuwapo kwa baadhi ya wajumbe walioomba kuhamishwa kwenye kamati walizopangiwa awali, kumekuwapo na mazungumzo kati ya Kambi ya Upinzani Bungeni na kiti ofisi ya Spika juu ya suala hilo.
 
Inaelezwa kati ya wajumbe watakaohamishwa kutoka kwenye kamati zao za awali ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe analiyekuwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Jamii na sasa atapelekwa ya Hesabu za Serikali (PAC).
 
Naye Mbatia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, sasa atapelekwa kwenye Kamati ya Bajeti aliyokuwa akitumikia kwenye Bunge la 10.
 
“Mbali na kambi ya upinzani bungeni, kulikuwa pia na shinikizo la mataifa ya nje ambayo yanataka hizi kamati za kuangalia serikali ziongozwe na upinzani, jambo ambalo Spika pia alikuwa anataka lakini kwa sababu fulanifulani ikawa kama ambavyo tuliona kamati zimepangwa awa,” kilisema chanzo kimoja cha habari kilichotaka kutotajwa jina lake.
 
Spika wa Bunge, alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo kupatikana, kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
 
Naye Naibu Katibu wa Bunge, John Joel, alipotafutwa alisema suala hilo kama lipo halijafika mezani kwake.
 
“Kwa kweli siwezi kusema chochote kwa sababu hilo bado halijanifikia, lakini kama hayo mabadiliko yamefanywa ama yatafanywa na Spika ni sawa kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka kikanuni,” alisema na kuongeza:
 
“Kwa sababu kulikuwa na baadhi ya wabunge waliomba kuhamishwa kwenye kamati, sisi tulichokuwa tunafanya ni kupeleka kwa Spika kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwabadilisha.” 
 
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilah, alisema bado hajapata taarifa juu ya suala hilo na kutaka aulizwe Spika mwenyewe.
 
Juzi Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bunge, Tundu Lissu, alisema wanafikiria kumpeleka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kwenye kamati ya PAC ili awe mwenyekiti wao.
 
“Wasipokubali (kubadilisha wajumbe) hatutakubali ungozi tutaacha, mimi mwenyewe sheria ndogo siendi, huko ni kupoteza muda kwa sababu hakuna kamati ya ovyo vile, nitaenda sheria na katiba na kushiriki mijadala, kura tu ndiyo sintopiga, hoja yoyote ya kisheria ikiibuka bungeni nitaibuka na watashangaa,” alisema Lissu.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa