Home » » MWANASAIKOLOJIA ANT SADAKA AONGEA NA WANAWAKE WA DODOMA KWENYE MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI YANAYOENDESHWA NA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION

MWANASAIKOLOJIA ANT SADAKA AONGEA NA WANAWAKE WA DODOMA KWENYE MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI YANAYOENDESHWA NA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma yanayoendesha na Taasisi ya Manjano Foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa LAPF House.
Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake waDodomawanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano Foundation na mkufunzi wa maswala ya Biashara mjini Dodoma yanayoendelea kwa wiki nzima.
 Washiki Kutoka Mkoani Dodoma na Maeneo Jirani wakiliskiliza kwa Makini Wakati wa Mafunzo hayo Leo.
Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani, wajiamini, watambue vyeo vyao katika familia, wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Dodoma kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Dodoma kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. 
Picha ya Pamoja Washiriki hao kutoka Mkoani Dodoma wakiwa na Mwanasaikolojia Anti Sadaka Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions africa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.
Anti Sadaka amewashauri wanawake wasiache kujifunza na waache kujibweteka baada ya mafunzo haya kuisha isipokuwa wawe makini kutafuta elimu zaidi ya kujiongezea ujuzi katika kazi zao.








0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa