Home » » TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA DODOMA

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi  Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers  ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma kuanzia Jumatatu, tarehe 28 March 2016 kwenye ukumbi wa  LAPF House Mkoani  Dodoma. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Dodoma na mikoa ya jirani. 
Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliotuma maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi 2016 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa  LAPF House Mkoani Dodoma.
Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 
Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba ya bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa 
Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 712 646 322  au +255 718 010 107

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa