Home » » KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MRADI WA MABASI YA HARAKA.

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MRADI WA MABASI YA HARAKA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
KAMATI ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) unaotekelezwa mkoani Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza, alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba kamati imefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo baada ya kukagua miundombinu ya mradi unaosimamiwa na Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Alisema barabara, vituo vikuu na vidogo vimejengwa kwa viwango vilivyokusudiwa. Alisema hatua zilizobaki ni uwekaji mifumo ya nauli kwa njia ya kadi, kufunga mitambo ya kuongoza mabasi na kujenga uzio kwenye kila kituo kikubwa.
Alisema kukamilika kwa hatua za mwisho kutategemea uharaka wa serikali katika kutoa fedha zinazohitajika kuruhusu mabasi kuanza kufanya kazi. Rweikiza alisema kamati imeridhika kuwa mradi utakomboa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa utaondoa msongamano wa magari, utachochea ukuaji wa shughuli za uchumi na kwa hiyo kuboresha maisha ya watu.
“Tumeona mabasi yaliyoletwa ni mazuri, yataweza kubeba watu 80 na 150, pia yana kamera kwa ajili ya kudhibiti uhalifu na ajali,” alisema Rweikiza na kuongeza kwamba kamati imeshauri nauli ziwe nafuu watu wa vipato tofauti waweze kunufaika na mradi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utawala na Serekali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo, alipongeza kamati hiyo kwa kufanya ziara na kuzungumza na watendaji wa wakala huo na kupata ufafanuzi wa utekelezaji wake. “Kuna hatua ndogo ndogo zinafanyiwa kazi. Muda si mrefu wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wataanza kunufaika na maradi”, amesema Jaffo.
CHANZO: HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa