Home » » Polisi wabambikia kesi kuendelea kuadhibiwa

Polisi wabambikia kesi kuendelea kuadhibiwa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema polisi wanaothibitika kuwabambikia watu kesi huchukuliwa hatua zinazostahili ikiwemo kufukuzwa kazi, hivyo wananchi waelewe kwamba Serikali haifanyii mzaha suala hilo.
Alisema na kutoa mfano wa askari watatu waliofukuzwa kazi hivi karibuni baada ya kuthibitika kumbambikia mtu kesi gerezani.
Alisema; “Ninaomba kuweka suala hili vizuri kwamba si askari wote wanabambikia watu kesi na wala si jeshi lote la polisi linafanya hivyo. Wanaohusika ni wachache katika matukio machache na wanapothibitika huchukuliwa hatua stahiki.”
Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) aliyetaka kujua Serikali inachukua hatua gani kukomesha tabia ya askari wa Jeshi la Polisi kubambikia watu kesi.
Masauni alisema jamii inapaswa kuelewa kuwa Serikali haizembei kuchukua hatua pindi inapohitajika kufanya hivyo kwa askari yoyote anayebambikia mtu kesi.
Alikiri kuwa masuala hayo ya askari kubambikia watu kesi ni kweli yapo, ingawa alisema ni machache tofauti na inavyoelezwa.
Chanzo Gazeti La Habari Leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa