Na Tiganya Vincent, Dodoma.
Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.
Alisema
kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji
wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne
ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada
lilipo katika mto Rufiji.
Kuhusu
kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo , Waziri Mkuu
alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari
katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa
sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa
kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa hali
hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa
Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.
UPUNGUFU WA SUKARI.
Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.
Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu
huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa
Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na
hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.
Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika.
Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.
Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kutoka zinapoagizwa na kumfikia mlaji.
WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU LUMBESA
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amesema kuwa ni kosa kwa wanunuzi wa mazao
ya wakulima kununua mazao kwa vipimo visivyo halali ambavyo
havikuidhinishwa na Wakala wa Vipimo nchini.
Amewaagiza viongoizi wote wa Halmashauri,Wilaya na Mikoa yote nchini kuhakikisha wakulima hawanyonywi kupitia wananunuzi mazao kuliko vipimo halisi kama vile Lumbesa.
Mhe.
Majaliwa amewaagiza Kamati za Ulinzi na Usalama katika za mikoa na
wilaya kusimamia zoezi hili ili mkulima alipe kwa vipimo halali ambavyo
ni kilo au gunia liloshonwa kiwanda na sio lile liloongezewa
kichuguu(lumbesa).
ELIMU YAONGEZA IDADI YA WATOTO WANAOINGIA LA KWANZA
Kuhusu
suala la elimu bure, Waziri Mkuu amesema kuwa lengo ilikuwa na lengo la
kumpunzia mzazi mzigo wa ada ya shule za Msingi na Sekondari.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa ada hizo zilikuwa ni kati ya shilingi elfu 20 na elfu 70.
Amesema kuwa sehemu imebebwa na Serikali ni pamoja na maji,ulinzi,umeme na gharama za mitani mbalimbali.
Aidha,
Mhe. Majaliwa alisema kuwa baada ya mpango huo wa elimu bure kumekuwepo
na ongezeko kubwa na watoto waliondikishwa kujiunga darasa la kwanza
mwaka huo na hivyo kusababisha changamoto ya upungufu wa madawati na madarasa.
Alisema
kuwa Serikali inaendelea kuzifanyia changamoto hizo na kutoa wito wadau
mbalimbali kuungano mkono juhudi hizo za Serikali.
0 comments:
Post a Comment