Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
WATANZANIA
ambao wanapenda kutembelea nchi ya Uingereza wametakiwa kuzingatia
taratibu zilizowekwa na nchi hiyo katika maombi ya viza ikiwemo kuomba
viza mapema, kuwasilisha nyaraka zote muhimu pamoja na taarifa sahihi
ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.
Ushauri
huo umetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha ambaye alijibu swali kwa niaba
ya Waziri mwenye dhamana katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine
Mahiga lililotaka kujua ni sababu zipi zinazoifanya Serikali ya Tanzania
iridhike na utaratibu unaoleta usumbufu kwa Watanzania wanaotaka
kusafiri kwenda Uingereza kutafuta viza kupitia Kenya na Afrika Kusini.
Mhe.
Ole Nasha ameeleza kuwa, hapo awali huduma za viza zilikuwa zikitolewa
na Ubalozi wa Uingereza nchini, Ubalozi huo ulihamisha shughuli za
utoaji wa viza kutoka hapa nchini kwenda nchini Kenya tarehe 1 Desemba,
2008 na kuanzia tarehe 18 Agosti, 2014 huduma hizo zimehamishiwa nchini
Afrika Kusini na siyo Kenya tena.
Alifafanua
kuwa, kwa mujibu wa Serikali ya Uingereza uamuzi huo ni wa kisera ba
umefikiwa ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa Idara ya Viza na
Masuala ya Uhamiaji ya Uingereza.
“Mchakato
wa utoaji viza za Uingereza unafanyika Kikanda, kwa mantiki hiyo maombi
yote ya viza kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na Kati yanafanyiwa
kazi katika Ubalozi wa Uingereza nchini Afrika Kusini”, alisema Ole
Nasha.
Aidha,
Waombaji wa viza hapa nchini wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja
na nyaraka zinazohitajika katika Kituo cha Kuombea Viza (Visa
Application Centre) kilichopo Viva Tower, Dar es Salaam.
“Kituo
hicho ndicho chenye jukumu la kusafirisha maombi hayo kwenda Afrika
Kusini na kurejesha nyaraka husika kwa waombaji nchini, Mwombaji
halazimiki kufuata huduma hiyo nchini Afrika Kusini”, alisema Mhe. Ole
Nasha.
Amefafanua
kuwa, Ubalozi wa Uingereza Nairobi unashughulikia maombi machache ya
viza (restricted number of applications) kwa Viongozi wa Serikali na
watendaji wengine wenye pasi za Kidiplomasia hasa katika hali ya dharura
ambapo maombi hayo yanapaswa kupelekwa moja kwa moja Ubalozi wa
Uingereza Nairobi na waombaji wenyewe au kupitia Ubalozi wa Tanzania
Nairobi.
“Napenda
kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge pamoja na Watanzania wenzangu kwamba.
Zoezi la utoaji viza lina utaratibu Wake na moja ya taratibu hizo ni
kwamba nchi inayotoa Viza Ina Uluru wa kuamua ni wapi itatolea viza
hizo, kwa mantiki hiyo hata Serikali yetu ya Tanzania ku pitia Balozi
zake zilizopo nje inazo taratibu zake za kutoa viza kwa wageni wote
wanaotembelea Tanzania, ni vema Watanzania ambro wangependa kutembelea
nchi ya Uingereza wakazingatia taratibu zilizowekwa na nchi hiyo katika
maombi ya viza”, alisisitiza Ole Nasha.
0 comments:
Post a Comment