Home » » TANZANIA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MAAFISA UGANI 6,266

TANZANIA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MAAFISA UGANI 6,266

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Na Jonas Kamaleki
MAELEZO
Dodoma

Tanzania ina upungufu wa maafisa ugani 6,266 ambao serikali inahitaji kuajiri kadri ya upatikanaji wa fedha.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mkoa wa Kagera lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliva Semuguruka aliyetaka kufahamu mpango wa serikali katika kuwasaidia wakulima waweze kunufaika na kilimo cha Ndizi, Kahawa, Mahindi na Maharage.

“Mathalani mwaka 2006 wizara yangu ilibaini kuwa walikuwepo maafisa ugani 3,377, ukilinganishwa na mahitaji ya maafisa hao 15,022" alisema Dkt. Tizeba.

Aliongeza kuwa Serikali inajitahidi kusomesha vijana wengi kwenye vyuo vya kilimo na kuajiri maafisa ugani 5,377 na kufanya jumla ya wataalam kuwa 8,756 kwa sasa ambao wanatoa elimu na kanuni bora za kilimo.

Tizeba alisema Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, inaendelea kueneza matumizi ya vituo vya rasilimali za Kilimo vya Kata ambapo jumla ya vituo 322 vimejengwa katika Halmashauri 106 kwenye mikoa 20.

“Kati ya vituo hivyo vituo 224 vimekamilika na vinafanya ya kutoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji, mashamba ya majaribio, kutoa huduma kwa wafugsjio na matumizi ya zana za kilimo” alisema Dkt. Tizeba.

Aidha Waziri Tizeba aliongeza kuwa Wizara yake inaandaa na kurusha vipindi vya redio kuhusu kanuni za kilimo bora kupitia vituo mbalimbali vyas redio, ambapo kwa mwaka 2015/16 jumla ya vipindi 122 vilirushwa na vipindi 52 vilirushwa kupitia TBC Taifa na vipindi 70 vilirushwa kupitia redio jamii.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti MaaluM (CCM), Mhe. Oliver Semguruka aliyetaka kujua ni lini bei ya kahawa itapanda ili wakulima wasiuze nje ya nchi, Dkt Tizeba alisema bei ya kahawa itakuwa nzuri ikiondolewa kodi 26 zilizopo hivi sasa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa