By Godfriend Mbuya
Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga
amesema kwamba kitendo cha wabunge wa upinzani kususia vikao vya bunge
la bajeti lililopita kwa kisingizio cha kutokuwa na imani na Naibu Spika
Dkt. Tulia Ackson
''Wale vyama vya siasa wanataka kujijenga
kisiasa watajijenga kisiasa kwa namna gani , zile tunaziita sanaa za
kisiasa, kwa sababu naibu spika amechaguliwa na wengi na wengi ndani ya
Bunge ni wabunge wa ccm sasa wangewezaje kumtoa kirahisi na hana
mapungufu kama wanavyosema''Amesema Mlinga.
Bungeni kuna kanuni kama zilivyokuwa sehemu za kazi, Naibu Spika yupo vizuri sana katika kusimamia sheria
Sababu ambayo waliitaja ya kutoka nje
ilikuwa ni wanafunzi wa UDOM kufukuzwa chuo na hata ajenda hiyo ililetwa
na wabunge wa CCM kwa hiyo lengo lao ni kujijenga kisiasa.
''Asilimia 99% ya wabunge wa upinzani
walikuwa hawapendelei ile hali siyo kwamba sababu ya fedha tuu bali hali
ile ilikuwa inawadhalilisha'' ameongeza Mlinga
Bunge la 11 mkutano wa tatu uliomalizika
hivi karibuni Mkoani Dodoma wabunge wa upinzani walisusia vikao zaidi ya
wiki tatu ambavyo viliongozwa na naibu Spika kwa kusema kwamba hawana
imani naye.
0 comments:
Post a Comment