Home » » KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA

KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA

 Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku ya kwanza walipokutana wakati wa maandalizi ya kutengeneza kipindi hicho.
Mohammed Hammie na Happy Balisidya wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kufahamu watakuwa wakiendesha kipindi cha CHUKUA HATUA.
---
Chukua Hatua ni kipindi kipya cha radio kitakachowashirikisha vijana, wakizungumza na kujadili kwa pamoja masuala yanayowahusu hasa ya kujikwamua na maendeleo mkoani Dodoma na maeneo jirani.
Hiki ni kipindi ambacho kinatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za ajira kwa vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa vijana wa kike na kiume.
Lengo kuu la kipindi hiki ni kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira na changamoto wanazokutana nazo katika mihangaiko yao, kipindi kitapaza sauti za vijana ambazo hazikupata nafasi ya kusikika hapo kabla.
Si kipindi tu, bali pia ni jukwaa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi, mawazo, uzoefu na pia kujifunza kutoka kwa wengine, ni mahala pekee ambapo kijana atayaona matarajio na uzoefu kutoka fani na taaluma mbalimbali.
Kipindi pia kinatarajiwa kuimarisha ujuzi na kuelekeza upya akili za vijana kufanya kazi na kuchangamkia fursa za ajira kwa ujasiriamali, kujiajiri na kuukwepa umaskini uliokithiri miongoni mwao.
Kipindi kitaanza kuruka hewani siku ya Alhamisi ya tarehe 01/09/2016 kupitia kituo cha RASI FM RADIO inayopatika masafa ya 103.7 Dodoma.
Pia kipindi kitakuwa kinapatikana kupitia mtandao wa Youtube ukurasa wa CHUKUA HATUA, pia mijadala itakuwa inaendelea kupitia ukurasa wetu wa facebook ambao ni CHUKUA HATUA, Instagram ni KIJANA CHUKUA HATUA, na Twitter ni CHUKUA HATUA1
Kipindi hiki kimewezeshwa na mpango wa pamoja wa ajira kwa vijana wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kazi Duniani (ILO) kwa udhamini wa SIDA.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa