Home » » Majaliwa kuhamia Dodoma baada ya vikao vya Bunge

Majaliwa kuhamia Dodoma baada ya vikao vya Bunge




By Sharon Sauwa, Mwananchi ssauwa@mwananchi.co.tz
Dodoma. Serikali ya Mkoa wa Dodoma imeahirisha mapokezi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa yaliyokuwa yafanyike leo hadi hapo vikao vya Bunge vinavyoanza Jumanne wiki ijayo vitakapomalizika.
Akizungumza jana Mkuu wa Mkoa huo, Jordan Rugimbana alisema mkoa unajipanga namna ya kumpokea Waziri Mkuu baada ya vikao hivyo kumalizika.
Alisema kwa msingi huo mapokezi hayo hayatafanyika leo hadi vikao hivyo vitakapomalizika.
Hata hivyo, alisema ujio wa Waziri Mkuu mjini hapa bado uko palepale na kwamba maandalizi ya namna ya kumpokea yanaendelea.
Kamati za Bunge 12 zimekuwa zikiendelea na vikao vyake mjini Dodoma kwa wiki ya pili mfululizo.
Wiki iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme alisema Waziri Mkuu angepokelewa leo katika eneo la Mtumba kisha kuzungumza na wakazi wa Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri.
Uamuzi wa kuhamia rasmi Septemba Mosi ulitangazwa na Waziri Mkuu mwenyewe katika maadhimisho ya siku ya mashujaa Julai 25 mwaka huu yaliyofanyika mjini hapa.
Julai 26 aliunda kamati iliyoshirikisha taasisi mbalimbali na kuratibiwa na Rugimbana ili kuandaa mpango mkakati wa kuhamia Dodoma.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, kikosi kazi hicho
walibaini mjengo kwa ajili ya ofisi yanaweza kupatikana kwa asilimia 70 na nyumba za kuishi kwa asilimia 75.


 
Chanzo Gazeti la Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa