Home » » MHE.UMMY MWALIMU ALIAGIZA BARAZA LA FAMASIA KUFANYA OPERESHENI YA KUHAKIKI VYETI VYA WATAALAM WA DAWA (WAFAMASIA) NCHI NZIMA KUTHIBITI WAUZA DAWA FEKI NA KUWAFUTIA USAJILI WAFAMASIA WANAOUZA DAWA ZA SERIKALI.

MHE.UMMY MWALIMU ALIAGIZA BARAZA LA FAMASIA KUFANYA OPERESHENI YA KUHAKIKI VYETI VYA WATAALAM WA DAWA (WAFAMASIA) NCHI NZIMA KUTHIBITI WAUZA DAWA FEKI NA KUWAFUTIA USAJILI WAFAMASIA WANAOUZA DAWA ZA SERIKALI.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  Bodi ya Baraza la Famasia nchini.
 
Na.Mwandishi Wetu - Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Famasia nchini kuanza kazi ya kuhakiki vyeti vya wauza dawa (wafamasia) katika maeneo mbalimbali nchini ili kudhibiti na kuwaondoa wauza dawa wasio na sifa ya kufanya kazi  hiyo kwenye maduka ya dawa.

 Pia ameligiza Baraza hilo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kuwafutia usajili wafamasia wanaokiuka kanuni na taratibu za Baraza hilo ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya upotevu wa dawa na uuzaji wa dawa  na vifaa Tiba vya Serikali.

Mhe.Ummy alitoa maagizo hayo mjini Dodoma katika Kikao Chake cha kwanza na Bodi ya Baraza la Wafamasia nchini ambapo pamoja na mambo mengine alikemea utaratibu ulojitokeza wa kutaka kuifanya biashara ya dawa kuwa sawa na biashara nyingine za kawaida za maduka ya kuuza nguo jambo ambalo halikubaliki.

 "Biashara ya maduka ya dawa lazima iheshimiwe, lazima ianzishwe kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na watu wanaoajiliwa kuhudumia maduka ya dawa kuwa na sifa zinazotakiwa, kazi ya kuuza dawa za binadamu sio sawa na biashara ya kuuza nguo au viatu", alisema Mhe Ummy.

Ameliagiza  Baraza hilo kufanya operesheni nchi nzima  kukagua maduka yote ya dawa kubaini mapungufu yaliyopo kisha kuchukua hatua kali dhidi ya wale wataogundulika kufanya biashara hiyo bila kufuata taratibu na kuongeza kuwa baraza hilo ni lazima liendelee kupambana na watoa dawa wasio na sifa  na wale wasio waaminifu wanaotengeneza vyeti bandia vya Wataalam wa Famasi.
Pia ametoa maelekezo kwa baraza hilo  kuangalia suala la mgongano wa maslahi hasa pale ambapo Mfamasia wa Wilaya anatuhumiwa kumiliki maduka ya Dawa mawili hadi matatu ndani ya Halmashauri anayofanyia kazi.

"Ni lazima suala hili tulitafutue suluhish nimefanya ziara mikoani jambo hili nimelikuta, mimi sielewi na Wananchi wengi hawaelewi pale Mfamasia wa Wilaya anapokua na maduka ya dawa hadi matatu  na muda wote yana dawa wakati dawa hizo hizo hazipatikani katika vituo na Hospitali za Serikal, Kwa nini wananchi wasiwe na hisia kuwa dawa zile ni za Serikali? Baraza nileteeni mapendekezo ya kutatua hili. Alisisitiza Mhe Ummy.

Aidha,  ameliagiza Baraza hilo kuweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili nchi iwe na wanataaluma wenye uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu.

Akitoa taarifa ya Utendaji Msajili wa Baraza la Famasia Bi.Elizabeth Shekalaghe alieleza kuwa zipo changamoto wànazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo maduka mengi ya kuuza dawa kuendesha biashara hiyo bila ya kuwa na vibali vya biashaa pia kuwepo kwa wauza dawa wasio na sifa ya kufanya shuguli hiyo.

Pia alieleza mikakati iliyowekwa na barza hilo ili kuhakisha changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi ili kuhakikisha huduma za uuzaji dawa zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu ili kuhakikisha unora wa huduma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Bàraza là Famasia, Legu Ramadhani Mhangwa, amesema kuwa Baraza hilo limekuwa likifanya kazi zake  kwa kuzingatia sheria ili kufikia malengo liliyojiwekea na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa na Mhe Waziri pia kutatua changamoto ya  uwepo wa vyuo binafsi vinavyofundisha taaluma ya famasi kutokidhi viwango pamoja na nia ya serikali ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kada za dawa nchini. 

Pia Baraza hilo limeahidi kushughulikia uhaba wa wakufunzi mahususi katika vyuo vinavyofundisha kada za famasi katika ngazi ya cheti na diploma.

Kuhusu mgongano wa maslahi kwa watumishi wakiwemo watendaji wa Halmashauri na wale wanaosimamia na kutekeleza kazi za baraza katika ngazi za mikoa na halmashauri, Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Baraza litahakikisha linasimamia kikamilifu Kanuni za Maadili na Miiko ya Kitaalamu za 2015 ili kutatua changamoto hizo iliwemo upotevu wa dawa za Serikali.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa