Na Beatrice Lyimo- MAELEZO DODOMA
Serikali
itaendelea kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria katika kugawa eneo la
Jamhuri katika ngazi ya Mkoa na maeneo mengine ya Utawala.
Akijibu
swali la Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe lililohusu ongezeko la ukubwa
wa Serikali na Watumishi wake na uanzishwaji wa maeneo mapya, Waziri
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George
Simbachawene amesema kuwa uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala.
Maeneo
hayo ni pamoja na Mikoa, Wilaya, Majimbo, Tarafa, Kata, Vijiji, Mitaa
na Vitongoji kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya mwaka 1977 ambayo humpa
Waziri mweye dhamana ya Serikali za Mitaa madaraka ya kuweka utaratibu
wa kugawa maeneo hayo.
Simbachawene
alisema kuwa Serikali itaendelea kugawa maeneo ya utawala kwa
kuzingatia msingi na uhitaji wa wananchi, Katiba na Sheria zilizopo.
“Kama
nia ni kupunguza gharama, tuunganishe maeneo madogo ili viwe sehemu
moja kuwiana na maeneo makubwa, Serikali itaendelea kugawa maeneo kwa
misingi ya kuzingatia Katiba na Sheria zilizopo” alifafanua Waziri
Simbachawene.
Kuhusu
ongezeko la watumishi, Naibu Waziri TAMISEMI Suleman Jaffo alisema kuwa
idadi ya watumishi iliongezeka kutoka wastani wa watumishi 222,792 hadi
wastani wa watumishi 405, 314 kati ya mwaka 2000 hadi 2015.
Ongezeko hilo limesababisha bajeti ya mshahara kuongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 668.6 hadi trilioni 3.05.
Aidha,
Jaffo aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015
imeongezeka Mikoa mitano kutoka 21 hadi 26, Wilaya 114 hadi 139, Tarafa
521 hadi 558, Halmashauri 233 hadi 185, Kata 3,833 hadi 4,420, Vijiji
10,376 hadi 12,545, Mitaa 1,975 hadi 4,037 na Vitongoji 57,137 hadi 64,677.
Azma
ya Serikali katika mgawanyo huo ni kusogeza huduma karibu na wananchi
kwa kuzingatia uwezo wa nchi kiuchumi na kuendelea kuzingatia
utekelezaji wake.
0 comments:
Post a Comment