Na Sheila Simba,Maelezo.
14.9.2016
WAKALA
wa Jiolojia Nchini (GST) imezitaka Taasisi za Umma, Wizara na Idara za
Serikali kuwatumia Wataalamu wa jiolojia katika shughuli za ujenzi wa
ofisi za Serikali Mkoani Dodoma ili kuweza kukabiliana na athari za
matetemeko la ardhi yanayotokea mara kwa mara Mkoani humo.
Wito
huo umetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Nchini(GST)
Profesa Abdulkarim Mruma, wakati wa mahojiano yake na MAELEZO kuhusiana
na athari zitokanakazo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo matetemo ya ardhi hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali imepanga kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma.
“Nashauri
Serikali kutuma wataalamu kufanya utafiti ili kuangalia ni maeneo gani
yanafaa kujenga ofisi za Serikali na zinatakiwa zijengwe kwa mfumo upi
ili ziweze kuhimili matetemeko ya ardhi pindi yanapotokea” alisema
Profesa Mruma
Aliongeza kuwa hapo awali ujenzi wa magorofa mkoani humo ilikuwa mwisho ghorofa nne kutokana na mkoa huo kupitia na Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ambalo kusababisha matetemeko ya mara kwa mara.
Akizungumzia
kuhusu ujenzi wa maghorofa Mkoani humo, Prof. alisema magorofa
yanayotakiwa kujengwa yawe mapana na yenye kuzingatia ugumu wa nondo,
aina saruji inayotumika katika ujenzi na uimara wa jengo husika.
“Jengo
likiwa nyembamba na refu ni rahisi kupata madhara pindi tetemeko
linapotekea hivyo ni vyema watu wafuate ushauri wa wataalamu kabla
kufanya ujenzi na pia kuangalia maeneo yanayofaa kwa ujenzi” alisema
Prof Mruma
Aidha
ameongeza kuwa majengo yote yatakayojengwa yanatakiwa kuzingatia ubora
wa majengo kwa kutumia wataalamu badala ya kujenga bila kushirikisha
wataalamu.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment