Home » » MJADALA WA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WAENDELEO MJINI DODOMA CHINI YA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII.

MJADALA WA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WAENDELEO MJINI DODOMA CHINI YA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo imekutana na kuendelea na kuujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kuendelea kupitia kifungu kwa kifungu katika Muswada huo.

Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Peter Serukamba alisema wamekuta katika kikao hicho ikiwa ni muendelezo wa kupitia Muswada huo kwa makini kabla ya kupelekwa Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.

Aliongeza kuwa ni wakati kwa wajumbe kuendela kuujadili kutoa maoni yao katika kuuboresha Muswaada huo ili waweze kupeleka Muswada ambao utaleta Sheria iliyobora kwa mufaa ya tasnia ya habari na watanzania kwa ujumla.

“Wajumbe nawaomba tuujadili na kuuchambua Muswada huu kwa makini sana kwani sisi ndio watungaji wa sheria na tutuo maoni na marekebisho yatakaoufanya Muswada huu kuwtoa Sheria iliyo bora” alisisitiza Mhe. Serukamba.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau habari  kupitia barua pepe ya cna@bunge.go.tz.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa