Home » » Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini umepunguza idadi ya utoro mashuleni.

Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini umepunguza idadi ya utoro mashuleni.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na. Lilian Lundo-Dodoma.

Serikali kupitia mpango wa kuinua ubora wa Elimu Tanzania
(Education Quality Improvement Programme Tanzania- EQUIP-T) umepunguza kiwango cha utoro na idadi ya wanafunzi wasiojuakusoma na kuandika shule za Msingi mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa leo, Mjini Dodoma na Kiongozi  wa mpango huo Mkoa wa Dodoma Francis Liboy katika semina ya mawasiliano ngazi ya Wilaya na jinsi ya kupashana simulizi ya mabadiliko iliooandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na EQIP-T.
 
"Mradi wa EQUIP-T umewezesha walimu shule za msingi kupata mafunzo mbalimbali ya njia bora ya ufundishaji kea wanafunzi wa madarasa ya Awali mpaka darasa la Nne kujua kusoma,kuandika na kuhesabu kwa ufasaha na kwa muda mfupi," alifafanua Liboy.
 
Kutokana na mafunzo hayo kwa walimu idadi ya wanafunzi
wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu imepungua kwa kiasi kikubwa kwa mkoa wa Dodoma na wilaya zake kutokana na walimu kuwa na mbinu mbalimbali za ufundishaji.
 
Mpango huo pia umeweza kuifanya jamii kuona shule ni mali
yao hivyo jamii imekuwa mstali wa mbele kufuatilia
mahudhurio ya watoto wao hivyo kupunnguza utoro kwa
kiasi  kikubwa.
 
Kwa upande wake Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya ya
Mpwapwa Anderson Njolegwa amesema kuwa mpango huo umeweza kupunguza utoro katika Wilaya hiyo kutoka wanafunzi 828 mwaka 2013 mpaka wanafunzi 572 mwaka 2016 ambao wanaendelea kupungua kila siku.
 
Mpango wa EQUIP-T ni mpango wa miaka minne ambao
ulianza mwaka 2014 ukiwa na  dhamira ya kuinua ubora wa
Elimu Nchini ambapo mpaka sasa mpango huo upo katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara na Lindi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa