Home » » ‘Hakikisheni mali za vyama vya ushirika zinanufaisha wanachama’

‘Hakikisheni mali za vyama vya ushirika zinanufaisha wanachama’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha, amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kuhakikisha mali za vyama hivyo zinawanufaisha wanachama na kukuza uchumi wa chama.
Alisema uchumi ukikua utaviwezesha vyama hivyo kujitegemea, kujiendesha kibiashara na kurejesha umiliki kwa wanachama kulingana na maadili na misingi ya ushirika.
Aidha, aliiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika iweke mfumo maalumu wa kumbukumbu wa kufuatilia mali za vyama vya ushirika kuzilinda na kuhamasisha wananchi wa rika mbalimbali kujiunga.
Ole Nasha alitoa agizo hilo wakati akifungua kikao cha kazi cha siku tatu cha wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu, miradi ya pamoja na wa benki za ushirika nchini, kilichoanza jana mjini hapa.
Aliwataka viongozi hao kuhakikisha mali za wanaushirika zinalindwa kisheria kama vile kuwa na hati.
Aliwakemea wanaouza mali hizo kiholela kwa wenye mali na kutaka ushirika uendeshwe kwa uwazi na ufanisi. Alitaka wawapunguzie wanachama michango kwa ajili ya kuendesha shughuli za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi shirikisho na kuwa na vyanzo vya mapato vya ndani, ili kuondoa utegemezi wa mikopo.
“Ni muhimu kutambua na kuanzisha mpango mkakati wa kuongezea thamani mazao ya wanachama kama vile kuanzisha viwanda vidogo na vya kati. Hii itawaongezea kipato, ajira, kupunguza upotevu wa mazao na pia itakuwa ni mchango wenu katika kutekeleza azma ya serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda,” alisema Ole Nasha.
Aidha, aliiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika iweke mfumo maalumu wa kumbukumbu wa kufuatilia mali za vyama vya ushirika ili kuzilinda dhidi ya ubadhirifu na upotevu, kuweka na kuimarisha huduma ndani ya vyama vya ushirika ili kuvutia wananchi wa rika mbalimbali kujiunga.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa