Home » » SBL yatoa elimu kuhusu unywaji pombe kistaarabu Mkoani Dodoma

SBL yatoa elimu kuhusu unywaji pombe kistaarabu Mkoani Dodoma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, akitoa semina  elekezi kuhusu kampeni unywaji kistaarabu kampeni ambayo imezinduliwa mapema leo katika Hotel ya Morena mkoani Dodoma 

Meneja wa mauzo wa SBL  mkoa wa Dodoma Adam Nelson akiteta jambo na Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai katika mkutano uliokutanisha wadau mbali mbali katika mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu uliofanyika katika Hoteli ya Morena mapema leo mkoani Dodoma
Wadau mbali mbali kutoka mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistarabu uliofanyika mapema leo Morena Hoteli Mkoani Dodoma.

Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai akitoa hotuba   katika mkutano uliokutanisha wadau mbali mbali katika mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu uliofanyika katika Hoteli ya Morena mapema leo mkoani Dodoma
 Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akitoa maelezo kwa waandishi wa habari mara baada ya    uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu  katika mkutano uliokutanisha wadau mbali mbali kutoka mkoa wa Dodoma wakati wauliofanyika katika Hoteli ya Morena mapema leo mkoani Dodoma  

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya unywaji kistaarabu



Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha Akisaidiana na Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai na Meneja wa mauzo wa SBL mkoa wa  Dodoma Adam Nelson kuvisha kava la gari lenye ujumbe unaoendana na kampeni ya unywaji kistaarau iliyozinduliwa mapema leo Morena Hoteli Mkoani Dodoma.

Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu iliyozinudliwa na SBl mapema leo katika Mkoa wa  Dodoma.



 Dodoma , Novemba 9 , 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.  
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai, amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia  bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Nchai.
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Nchai.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia CP Nchai anasema “ama kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.  
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa