Home » » WATUMISHI WA UMMA 1,663 WACHUKULIWA HATUA MBALIMBALI ZA KINIDHAMU

WATUMISHI WA UMMA 1,663 WACHUKULIWA HATUA MBALIMBALI ZA KINIDHAMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma
Watumishi wa Umma 1,663 kutoka Wizara, Idara zinazijitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kubainika kusababisha watumishi hewa 19,629 hadi Oktoba 25, 2016.
Waziri ya Nchi, Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mainda Hamad Abdallah (Mbunge wa Viti Maalum) alilohoji hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watumishi wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Akifafanua idadi hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa idadi ya watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu kutoka Wizara mbalimbali ni 16, Idara zinazijitegemea na Wakala za Serikali watumishi tisa, Sekretarieti za Mikoa watumishi sita na Mamlaka za Serikali za Mitaa watumishi 1,632.
Waziri Kairuki amesema kuwa watumishi hao wameisabishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 19, huku Halmashauri ya Kinondoni ikiwa na watumishi hewa 107 ambao waligharimu Serikali sh. bilioni 1.29, Kishapu watumishi 73 wamesababisha hasara ya kwa kugharimu sh. milioni 543 na kuonya kuwa waajiri waendelee kuchukua hatua za haraka na kudhibiti uwepo wa watumishi hewa ili kuipunguzia Serikali kuingia hasara kubwa badala ya kuwahudumia wananchi.  
Aidha, Waziri Kairuki amesema kuwa jumla ya watumishi 638 wamefunguliwa mashtaka polisi, watumishi 50 wanafanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na watumishi 975 mashtaka yao yamefikishwa kwenye Mamlaka zao za kinidhamu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa