Home » » BARAKA DA PRINCE NA ROSE NDAUKA KUMSINDIKIZA MC.PILIPILI KATIKA TAMASHA LA CHRISTMASS, KIDS FESTIVAL , DODOMA

BARAKA DA PRINCE NA ROSE NDAUKA KUMSINDIKIZA MC.PILIPILI KATIKA TAMASHA LA CHRISTMASS, KIDS FESTIVAL , DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mc Pilipili
 Baraka Da Prince
Rose Ndauka 

MSANII wa kizazi kipya Baraka Da Price pamoja  na Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie, Rose Ndauka wamesema kuwa wamejiandaa vema kumsindikiza Mchekeshaji maarufu nchini , Emanuel

Matebe a.k.a Mc Pilipili  katika Tamasha la Chrismass la kids Festival litakalofanyika mkoani Dodoma

katika viwanja vya Nyerere Square Desemba 25 na 26 mwaka huu.

Wasanii hao pia Desemba 26 mwaka huu watatoa burudani nyingine kama hiyo katika ukumbi wa royal village na kuwapa fursa watu wa Dodoma kupiga picha na Tuzo aliyoipata Mc.Pilipili  ya  Mshereheshaji bora wa mwaka 2016.

Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari,Muigizaji nguli Rose Ndauka alisema kuwa  tamasha hilo litakuwa  la kipekee katika mkoa wa Dodoma  ambapo ataweza kupanda jukwaani pamoja na Mchekeshaji huyooo na kutoa burudani ya aina yake.

Alisema  pia ataamua kuongea ukweli juu ya uhusiano wake na Mc Pilipili katika tamasha hilo kwani  watu wengi wamekuwa wakiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya ukaribu waliokuwa nao.

"Nataka kuwaambia watu wangu wa Idodoma kule kwa kina Mc.Pilipili mkae tayari kwa ujio wangu kwani siku hiyo ndio itakuwa siku yangu maalum ya kupanda jukwaani na Mc.Pilipili katika kuhakikisha nina wavunja mbavu,Mashabiki zangu naombeni mjitokeze kwa wingi kuitikisa siku hiyo

Dodoma na viunga vyake,"alisema Kwa Upande wake Emanuel Matebe a.k.a Mc Pilipili alisema tamasha hilo litakuwa ni tamasha la aina yake kwani litawakutanisha wasanii mbalimbali nchini wa muziki wa kizazi kipya pamoja na waigizaji wakiwemo Baraka da Price,Rose Ndauka ,Katarina Karatu pamoja na Casto .

Alisema katika  tamasha hilo Decemba 25 mwaka huu watoto wataweza kuingia kwa kiingilio cha  shilingi 2000 huku wakubwa sh.5000 huku katika tamasha la Desemba 26,kutakuwa na kiingilio cha  VIP ikiwa 30000 na kawaida 10000.

"Nawakaribisha ndugu zangu wa Dodoma katika matukio haya mawili siku hiyo itakuwa siku ya

pekee kwangu kuonyesha kipaji changu nyumbani hivyo nitahakikisha nawatendea haki ipasavyo huku nikirudisha tuzo ya Mshereheshaji bora nyumbani niliyopewa katika  tuzo za Insta  Award  ambayo mashabiki zangu watapata fursa ya kupiga nayo picha,"alisema 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa