Home » » NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU, ANTHONY MAVUNDE AONGOZA MATEMBEZI YA UHAMASISHAJI WA UMMA KUHUSU UMUHIMU WA AFYA YA KINYWA NA MENO JANA

NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU, ANTHONY MAVUNDE AONGOZA MATEMBEZI YA UHAMASISHAJI WA UMMA KUHUSU UMUHIMU WA AFYA YA KINYWA NA MENO JANA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
  Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akizungumza mara baada ya kuongoza matembezi ya uhamasishaji wa Umma kuhusu umuhimu wa Afya ya Kinywa na Meno leo machi 19, mwaka huu Mjini Dodoma katika eneo la Nyerere Square ambapo kilele cha wiki ya afya ya kinywa na meno Tanznaia na maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno duniani yanatarajiwa kufanyika machi leo  20. eneo hilo na mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa  Waziri, ofisi ya rais, TAMISEMI ,  Mhe George Simbachawene,
 Meneja wa Benk Tawi la NMB Dodoma, Rehema Nassib (wa pili kushoto) akimsikiliza kwa makini mgeni rasmi alipokuwa akizungumza katika eneo la Nyerere square mara baada ya matembezi ya uhamasishaji wa Umma kuhusu umuhimu wa Afya ya Kinywa na Meno leo, kuanzia kulia ni Daktari wa Kinywa na Meno Hospitali ya Huruma CDH ya Mkoani Kilimanjaro Sr, Benjamine Buya, Mwalimu, Ingnatia Masinde na kushoto ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Al-Misbahul Muniyr International Society Foundition (AMISF), Mussa Kazimiry
 Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde (wa tatu kulia) aongoza matembezi ya uhamasishaji wa Umma kuhusu umuhimu wa Afya ya Kinywa na Meno leo mjini Dodoma katika eneo la Nyerere square ambapo kilele cha wiki ya afya ya kinywa na meno Tanznaia na maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno duniani yatafanyika leo  katika eneo hilo,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Mhe, George Simbachawene, Waziri, ofisi ya rais, TAMISEMI 
Wakiwa katika Maandamano katika baadhi ya Barabara za Dodoma
Bendi ya Askari ya JKT Makutupora Dodoma ikiongozwa na Afisa Mteule Daraja la Pili  (WO2) , Dafroza Pesambili  ikipita mbele ya mgeni rasmi baada ya kumaliza matembezi hayo
Mgeni rasmi,  Anthony Mavunde (wa tatu kushoto) akipokea maadamano hayo
Mkuu wa Wilaya, dodoma, Christina Mndeme akisalimia wananchi na wadau walioshiriki matembezi hayo, kushoto ni naibu mwenyekiti wa bodi ya wa dhamini wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Halima Mamuya
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) na daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha restorative dentistry, MUHAS. akitowa utambulisho wa msafara wa Mataktari  wake alioongozana nao
Wanafunzi wa Sekondari ya Dodoma wakicheza kwaito baada ya maadhimisho hayo
Baadhi ya Madaktari na wananchi wakisikiliza kwa umakini
Daktari wa Kinywa na Meno Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo, Dkt. Samwel Seseja akizungumza jambo baada ya matembezi hayo
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na Madaktari na viongozi mbalimbali
Wanafunzi wa Sekondari ya Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja baada ya matembezi hayo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa