Home » » SERIKALI YAWAHIMIZA WANANCHI KUCHANGAMKIA MIFUKO YA UWEZESHAJI KIUCHUMI NCHINI.

SERIKALI YAWAHIMIZA WANANCHI KUCHANGAMKIA MIFUKO YA UWEZESHAJI KIUCHUMI NCHINI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Wete Mhe.Mbarouk Salum Ali leo Bungeni MJini Dodoma katika Kikao cha thelathini na sita cha bunge la 11.

“Nakubaliana na Mhe.Mbunge  kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo lakini bado kuna upungufu wa maziwa,ambapo takwimu za makadirio za mwaka 2016 zinaonyesha  lita bilioni 2.09 za maziwa zilizalishwa na unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka ulifikia lita 47 ukilinganisha na lita 200 zinazopendekezwa na Shirika la chakula Duniani(FAO)”,Alisema Mhe.Tizeba

Aidha kati ya Ngombe milioni 28.4, Ngombe rasmi wa maziwa ni 782,995 tu sawa na asilimia 3 ya Ng’ombe wote.Aidha kati ya mbuzi milioni 16.7 ni mbuzi rasmi takribani 50,000 ndio wa maziwa ambao ni asilimia 0.3 ya mbuzi wote.

Amezitaja jitihada ambazo Serikali imechukua ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini ni pamoja na kumarisha mashamba ya kuzalisha mifugo ya Serikali (LMU’s) ili kuongeza idadi ya Ng’ombe wenye uwezo wa kuzalisha maziwa kwa wingi.
Aidha  Serikali imeanzisha vituo vya uhimilishaji katika kanda 6 hapa nchini ambazo ni kanda ya Ziwa(Mwanza),kanda ya Magharibi(katavi),Kanda ya kati(Dodoma),Kanda ya Mashariki(Kibaha),Kanda ya Kusini(Lindi) na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya) kwa lengo la kutoa huduma ya uhilimishaji wa Ng’ombe wa Maziwa walioko kwenye maeneo hayo pamoja na Ng’ombe wa Asili ili kuzalisha idadi kubwa ya Ng’ombe wa Maziwa.

Amehimiza kuwa Jitihada hizi zitawezesha idadi ya Ng’ombe wa Maziwa kufikia milioni 2.9 ifikapo mwaka 2021/22 ambao pamoja na ng’ombe wa asili wataweza kuzalisha lita bilioni 3.8 za maziwa.

“Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza katika uzalishaji wa mitamba ya maziwa na mashamba ya ng’ombe wa maziwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa maziwa hapa nchini”,Aliongeza Mhe.Tizeba

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa