Home » » MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.

MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu kwa wananchi.

.Mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago.


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde ameendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo leo amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero ya maji katika kijiji cha Matumbulu.

Mavunde amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero hiyo kwa kutoa mabomba ya kusambazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Kilomita 1 yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 8.

Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo, wananchi hao walishikwa na butwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo ilikuwa ya muda mrefu hali iliyosababisha wananchi kutumia maji yasiyo safi na salama.

Wananchi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Matumbulu Alfred Malogo, amefurahishwa na utekelezaji wa ahadi hiyo na kwamba alichokifanya Mavunde kuwapatia wakazi wa kijiji hicho mabomba kwa ajili ya kusambazia maji kitatatua kero yao ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa