Home » » MDEE ‘KORTINI’ KWA KUMDHALILISHA SPIKA

MDEE ‘KORTINI’ KWA KUMDHALILISHA SPIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Imeandikwa na Anastazia Anyimike, Dodoma

BUNGE limeagiza Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), kuitwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa kutokana na utovu wa nidhamu kwa kauli za kumdhalilisha spika.
Agizo la Spika limetolewa ikiwa ni siku moja tangu Mdee awekwe ndani kwa saa 48 na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ally Salum Hapi kwa kutoa kauli ya kumdhalilisha Rais John Magufuli.
Mdee na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya pia wa Chadema wanatumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi cha mwaka mmoja. Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza kabla ya kuahirisha shughuli za Bunge juzi jioni, alisema Halima amekuwa akimdhalilisha Spika katika mitandao ya kijamii.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa