Home » » TAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI WA AWAMU YA PILI KUFANYIKA MWEZI AGOSTI, 2017

TAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI WA AWAMU YA PILI KUFANYIKA MWEZI AGOSTI, 2017

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na: Veronica Kazimoto
Dodoma
18 Julai, 2017.
Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili unatarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya wadadisi yanayoendelea kufanyika mkoani Dodoma Meneja  wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira amesema  lengo kuu la utafiti huo ni kufuatilia viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza ili kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyotokea.

"Utafiti huu ni wa kitaifa na utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyojitokeza kwenye viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza", amesema Mwingira.

Nae Mratibu wa utafiti huo Rainer Kiama amesema kuwa utafiti huu unafanyika ili kutathmini kama mpango unaleta manufaa yaliyokusudiwa katika ngazi ya kaya kwa kutumia viashiria kama vile elimu, afya, kazi na matumizi ya muda, shughuli za kaya zisizo za kilimo, mapato, mikopo, akiba na uhamishaji fedha.

Viashiria vingine ni  shughuli za kilimo,  makazi ya kaya na upatikanaji wa maji, matumizi na usalama wa chakula katika  kaya, maamuzi katika kaya, ukatili kwa wanawake na matarajio ya vijana, mahusiano ya kaya na jamii pamoja na mtazamo wa kaya kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili utahusisha kaya takribani elfu saba (7,000)  ambazo zilihojiwa katika utafiti wa awamu wa kwanza uliofanyika mwezi Juni, 2015.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa