Home » » WAWEKEZAJI MADINI SASA KUTUMIA LESENI

WAWEKEZAJI MADINI SASA KUTUMIA LESENI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Imeandikwa na Anastazia Anyimike, Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi

SERIKALI imesema mikataba iliyopo ya madini ni ya mwisho na kuanzia sasa wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hiyo watatumia leseni.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mjadala wa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali ya Mwaka 2017, Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi alisema sheria hii mpya ikisainiwa itabadilisha mfumo huo kutoka kwenye mikataba na kuwa mfumo wa leseni.
“Tutafanya marejeo ya mikataba iliyopo, itatolewa taarifa ya mapitio hayo kwa Bunge, sasa ungeendelea na mikataba ina maana tungekuwa tumevunja hiyo mikataba. Sisi tunasema njooni kwa majadiliano, na niseme hii ndio mikataba ya mwisho sheria hii ikipita hakuna tena mikataba na hakuna leseni, hakuna mwekezaji ambaye atakuja baada ya sheria hii...
“Hiki kiporo cha mikataba baada ya hapo tunakwenda kwenye leseni. Ndio maana hao hawataweza kutuburuza kwenye mahakama za usuluhishi kwa sababu mikataba yao hatujaivunja, ila tumesema njooni tuzungumze. Lakini tuzungumze nini? Hapo tunaangalia mambo ambayo hayakubaliki,” alieleza Profesa Kabudi
CHANZO HABARI LEO
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa