Home » » NANENANE IWE NA FAIDA INAYOONEKANA KWA MKULIMA, MFUGAJI NA KILA MSHIRIKI- DKT NCHIMBI.

NANENANE IWE NA FAIDA INAYOONEKANA KWA MKULIMA, MFUGAJI NA KILA MSHIRIKI- DKT NCHIMBI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionja asali katika moja ya mabanda ya maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama bidhaa za mbogamboga katika banda la Wilaya ya Kondoa katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mkoa wa Singida katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionyeshwa shamba la mahindi lilostawi vizuri katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Julius Sang’udi alipotembea banda la jeshi la magereza kujionea bidhaa wanazotengeza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoka katika banda la Tume ya taifa ya Umwagiliaji, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.

Maonyesho ya nane nane yanatakiwa kuweka alama chanya na kuwa na sura ya mabadiliko yanayoonekana kwa macho kwa wakulima na wafugaji wanaoshiriki pamoja na wananchi wanaopata huduma na bidhaa katika maonyesho hayo.
Mgeni rasmi katika Ufunguzi wa maadhimisho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Chimbi ametoa rai hiyo mapema jana kwa wakulima, wafugaji na washiriki wakati akifungua rasmi maonyesho hayo huku akiwataka washiriki hao kuitumia fursa hiyo kwa manufaa zaidi.
“Ni vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa washiriki mliojitokeza katika kuonesha bidhaa zenu mbalimbali na pia kwa wale wote waliofika kwaajili ya kununua au kupata maelezo ya matumizi ya bidhaa hizo, wapate kitu tofauti kitakachooneka katika maisha yao”, amesema.
Dkt Rehema Nchimbi ambaye ametumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo na ufugaji wenye tija ili kuendana na falsafa ya serikali ya awamu ya Tano inayo himiza zaidi Uchumi wa Viwanda.
Aidha ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani na nje ya Nchi wafike kuwekeza katika mikoa ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa kila atakayekuwa tayari kuwekeza katika Mikoa hiyo.
 “Nimepita kwenye banda la Jeshi la Magereza na kuona bidhaa nyingi sana zilizotengenezwa na Ngozi na wamenihakikishia kuwa kiwanda chao kina uwezo wa kununua ngozi yote inayopatikana katika Mikoa ya Singida na Dodoma hivyo ni vizuri tutumie hiyo kama fursa” ameongeza Dkt Nchimbi.
Dkt Nchimbi amesisitiza kuwa Mikoa ya Singida na Dodoma haina ukame na ndio maana hivi sasa ameanzisha mpango maalum wa kilimo cha umwagiliaji kwakuwa watafiti wamewahakikishia kuwa mikoa hiyo ina kiwango kikubwa cha maji ardhini huku yakiwa karibu na uso wa ardhi.
Pia amewataka wananchi wa Mikoa ya Singida na Dodoma kuacha kabisa kukata miti kwa kisingizio cha kujikwamua kiuchumi kwasababu kuna njia nyingi sana za kuondokana na hilo badala ya kuharibu misitu.
“Kule Singida nimeanzisha kampeni inayojulikana kama ‘ACHIA SHOKA, KAMATA MZINGA’ ambayo  inampa mwananchi nafasi ya kuamua kuacha kukata mti na badala yake anafuga nyuki jambo linalomsaidia kujikwamua kiuchumi kwa muda mrefu zaidi kwasababu unaweza kuukata mara moja tu lakini mzinga unaweza kuutundika mara nyingi kadri uwezavyo”.
Dkt. Nchimbi alimalizia hotuba yake kwa kuwasisitiza maafisa kilimo kupeleka kalenda za kilimo katika ngazi zote kuanzia ngazi ya kijiji ili iwe rahisi kwa Mkulima kujua aina ya mazao anayoweza kulima kwa Mwaka husika badala ya kumsubiri Mkulima apate madhara kwanza ndipo aje apewe elimu ya mazao aliyotakiwa kulima kwa mwaka husika.
Maadhimisho ya 21 ya Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama NANENANE yamefunguliwa rasmi tarehe 3 Agost 2017 kwa kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Singida na Dodoma.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa