Home » » NG’OMBE WAWA KIVUTIO NANENANE

NG’OMBE WAWA KIVUTIO NANENANE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma
MAONESHO ya saba ya kitaifa ya mifugo juzi yalitia fora katika uwanja wa maonesho ya kilimo Nzuguni Dodoma kutokana na mifugo iliyoletwa kwenye maonesho hayo kuwa na afya nzuri na wenye kutoa maziwa mengi.
Miongoni wa vivutio hivyo ni ng’ombe dume aliyepewa jina la Mang’wengw’e ikiwa na maana ya mtemi. Ng’ombe huyo ni mchanganyiko wa golani na ng’ombe wa asili, ambapo ng’ombe huyo ni chifu katika kijiji cha Kapiti Kata ya Mhalala Wilaya ya Manyoni mkoani Singida Katika maonesho hayo yaliyozinduliwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba (pichani), wafugaji wa mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida na Pwani walipeleka mifugo yao katika maonesho hayo.
Miongoni mwa wafugaji walioleta mifugo yao Kedmond Makwayu kutoka Gulwe wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, alionesha ng’ombe wake mwenye mchanganyiko wa Mpwapwa na Golan mwenye uzito wa kilo 880 huku akitaja gharama ya kumpandisha ng’ombe jike ni Sh. 30,000 Pia mfugaji kutoka katika wilaya ya Chemba, Idris Noti alionesha ng’ombe dume aina ya Tengeru mwenye uzito wa kilo 450 mwenye miaka mitano ambaye mpaka sasa amezalisha ndama 20 na gharama za kupandisha jike ni Sh 10,000.
Mfugaji kutoka Itigi, Jihumbi Madeni alikuwa na ng’ombe wa asili mwenye kilo 550. Aidha ng’ombe kutoka Ranchi ya Kongwa ambaye ni dume mwenye jina la Mahinyika mwenye kilo 790 ambaye mpaka sasa amezalisha zaidi ya ndama 200. Mfugaji Valentino Kombo kutoka Kongwa alikuja na ng’ombe dume mwenye uzito wa kilo 970.
Mfugaji kutoka ranchi ya Rushu iliyopo Kisarawe Pwani alikuja na ng’ombe mwenye kilo 831 huku Taasisi ya Utafiti ya Tarili Mpwapwa ikija na ng’ombe aina ya Singida white mwenye kilo 450 na Iringa Red mwenye kilo 360.
Pia ng’ombe kutoka kampasi ya Mpwapwa aliyepewa jina la mkufunzi wa Chuo hicho, Kitinga mwenye kilo 430 na ana uwezo wa kutoa lita 21 za maziwa kwa siku. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya KIlimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Mary Mashingo alisema Tanzania ina rasilimali kubwa ya mifugo na kutaka wafugaji kubadilika na kufuga kisasa.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa