Home » » WATATU WAFARIKI KWA AJALI ZA BARABARANI DODOMA

WATATU WAFARIKI KWA AJALI ZA BARABARANI DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. WATU watatu wamefariki dunia papo hapo na mmoja kujeruhiwa baada ya magari matatu kugongana katika barabara ya Dodoma-Morogoro katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 9 usiku katika eneo la Chinangali II, Kata ya Buigiri, jirani na shamba la zabibu wilayani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alisema imehusisha magari matatu yaliyokuwa yakitokea Morogoro kuelekea Dodoma.
Alisema chanzo cha ajali ni mwendokasi wa magari mawili madogo ambayo yaligonga lori kwa nyuma.
Kamanda Mambosasa alisema lori lenye namba T 572 CAG na T 537 BXV aina ya Volvo lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dodoma likiwa na mzigo wa saruji, liligongwa kwa nyuma na gari lenye namba T 746 AQC Toyota LC lililokuwa linaendeshwa na Padri Antony Mashaka (45).
“Wakati tunatathmini ajali hiyo, lilitokea gari jingine la tatu lenye namba T 396 DHA Toyota Fontana na kuligonga lori tena kwa nyuma.
“Baada ya gari hilo kuligonga lori, lilipinduka na kusababisha vifo vya abiria watatu waliokuwamo.
“Lakini, dereva alikimbia ingawa ndani ya gari hilo kulikuwa na maiti za watu watatu wanaume wanaodaiwa kuwa ni abiria waliopandia Msamvu, Morogoro kwa mujibu wa abiria mmoja aliyepata majeraha kidogo usoni aitwaye Ramadhani Mlawa (28), mkazi wa Mwembe Songo Morogoro.
“Kwa hiyo, hata majina ya marehemu bado hayajafahamika na miili imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa