Home » » WAZAZI NA WALEZI WAENDELEA KUMIMINIKA KWENYE VIWANJA VYA NANENANE KUSAJILI WATOTO NA TOTO AFYA KADI YA NHIF

WAZAZI NA WALEZI WAENDELEA KUMIMINIKA KWENYE VIWANJA VYA NANENANE KUSAJILI WATOTO NA TOTO AFYA KADI YA NHIF

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bi.Anjela Mziray akikabidhi kadi kwa mmoja wa wazazi waliokuja kusajili watoto wao kwenye Huduma ya Toto Afya Kadi, katika viwanja vya Nzuguni kwenye maonesho ya Nanenane mkoani Dodoma.
Meneja wa NHIF Mkoani Dodoma Bi. Salome Manyama akielezea huduma ya Toto Afya Kadi kwa wazazi na walezi waliotembelea banda la NHIF kwenye maonesho ya Nanenane Nzunguni mkoani humo.
Baadhi ya maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakitoa Elimu kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika maonesho ya Nanenane Mkoani Dodoma kwenye viwanja vya Nzuguni.

Baada ya kuzinduliwa rasmi kwa huduma ya Toto Afya Kadi na Mheshimiwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, wazazi na walezi wameendelea kumiminika katika viwanja vya maonesho ya Nanenane katika Mikoa mbalimbali. Haya yamethibitika kwenye viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma ambapo watoto wameendelea kusajiliwa na kupata kadi za NHIF kwa mchango wa shilingi 50,400 tu kwa mwaka.

Akiongelea hili Meneja wa NHIF Mkoa wa Dodoma Bi.Salome Manyama amesema tunaendelea kusajili watoto na huduma ya Toto Afya Kadi na tunaendelea kuhimiza jamii kuhakikisha wanatumia fursa hii ili watoto wao wawe na uhakika wa matibabu.


Mtoto mwenye chini ya umri wa miaka 18 anasajiliwa na huduma hii ya Toto Afya Kadi kwa mchango wa 50,400 tu kwa mwaka, na atapata huduma zote za matibabu zinazotolewa na NHIF katika vituo vyote vilivyosajiliwa Tanzania nzima.


Mmoja wapo wa wazazi aliesajili watoto na huduma hii Bw. Kessy amesema anashauri wazazi wenzake na walezi kwa ujumla kuchangamkia fursa hii kwani ugonjwa haupigi hodi hivyo mtoto akiwa na uhakika wa Bima ya Afya hata Familia inakua na amani.

3 Attachments

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa