Home » » WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFANYA MABADILIKO KWA BAADHI YA WATENDAJI WAKE

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFANYA MABADILIKO KWA BAADHI YA WATENDAJI WAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  KATIKA kuongeza ufanisi kwenye utendaji, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amefanya mabadiliko ya baadhi ya watendaji kwenye wizara na idara zilizo chini ya wizara hiyo.

Mabadiliko hayo madogo yamegusa Chuo Cha Taifa cha Utalii, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) na Idara ya Utalii kwenye makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Akitangaza mabadiliko hayo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, Waziri Maghembe alimtaja Deogratius Mdamu kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Zahoro Kimwaga TAWA kukaimu nafasi ya Mkuu wa Shughuli za Utaliiwa Picha.

Profesa Maghembe alisema pia amemteua Phillip Chitaunga, kuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Maendeleo ya Utalii kwenye makao makuu ya wizara, ili kujaza nafasi iliyoachwa na Uzeeli Kiangi aliyestaafu utumishi kwa mujibu wa sheria.

"Kwenye Chuo chetu cha Taifa Utalii, ninamteua Dk. Shogo Mlozi kuwa Kaimu Mkuu wa Chuo ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Utalii na Ukarimu kwenye Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)," alisema.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa