Home » » WIZARA YAKUTANA NA WADAU KUDURUSU SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA NCHINI.

WIZARA YAKUTANA NA WADAU KUDURUSU SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA NCHINI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Erasto Ching’oro WAMJW
 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na  wadau wa masula ya jinsia mkoani Dodoma wanaokutana kudurusu Sera ya Mendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 ili kuiboresha kwa kuzingatia mazingira na mahitaji ya sasa.
Akifungua kikao hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Bibi Sihaba alisema kuwa ushiriki wa wadau kutoka ngazi ya Halmashauri ni wa muhimu ili kuibua maoni ya wananchi yatakayosaidia kuboresha sera iliyopo ili kuweza kuzingatia changamoto zinazowakabili wanawake katika maeneo ya mijini na vijijini ili kufanikisha azama ya Taifa ya kuwa na maendeleo endelevu kwa wanawake hapa nchini.
“Nyinyi ni Wadau muhimu na ndio mnaosimamia utekelezaji wa Sera na mkikakati ya Sera katika ngazi ya mkoa na Halmashauri maoni na changamoto mnanazotukutana nazo ni muhimu ili kujumuisha katika kipindi hiki cha kuhuisha Sera hii” alisema Bibi Sihaba.
Akiongea katika kuwasilisha mada elekezi, Mtaalamu Mwezeshaji Prof. Linda Mhando amesema Sera pendekezi itawezesha kufanya tathimi itakayotoa mwelekeo kuona kuwa mipango na mkakati mbalimbali inazingatia mambo muhimu yanayohimiza jamii kuachana na mitazamo ya kuwatambua wanawake peke yao, na badala yake kutambua ushiriki wa wanaume kama wadau muhimu katika Sera hii.
Pro Linda, aliongeza kuwa Sera inayopendekezwa itahimiza ushiriki sawa wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi, upatikanaji wa haki sawa kwa wanawake, uwepo wa hifadhi za jamii, kupunguza mzigo wa kazi, kuwashirikisha wanawake katika shughuli za kiuchumi na kuwahusisha wanawake katika fursa mbalimbali ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
Akizungumaza katika kikao hicho Bi. Dafrosa Sanga Mchumi Wizara ya Maliasili na Utalii alibainisha kuwa sera hii iwanufaishe wavulana na wasichana, wanawake na wanaume kwani hivi sasa watoto wengi wa kiume ndio wanaoathiriwa zaidi na utoro shuleni na maisha ya mitaani ukilinganisha na watoto wa kike. Wadau wameipongeza Wizara kwa uamauzi wake wa kuwashiriukisha wadau wa ngazi zote ili kupanua wigo wa maoni katoka ngazi mbali mabli kwa ajili ya umiliki wa sera hiyo na uzingatiaji wa haki kijinsia.
Maoni ya wadau yatakuwa msingi wa kuboresha Sera iliyopo ili kuimarisha uandaaji wa sera inayokidhi upatikanaji wa haki za wanawake na wanaume katika ngazi mbalimbali.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa