Home » » FAINALI YA BAHATI NASIBU YA SHINDA NYUMBA YA GLOBAL PUBLISHERS - MSOMAJI KUTOKA DODOMA AIBUKA MSHINDI

FAINALI YA BAHATI NASIBU YA SHINDA NYUMBA YA GLOBAL PUBLISHERS - MSOMAJI KUTOKA DODOMA AIBUKA MSHINDI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Diwani ya Kata ya Mabibo (aliyefungwa kitambaa machoni), akipelekwa na MC wa shughuli hiyo, Chaku kwenda kuchagua kuponi ya ushindi. Kazi ya kuchanganya kuponi ikiendelea. Mheshimiwa diwani akiwa ameshika kuponi ya ushindi, iliyotoka Gazeti la Championi. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza kwenye droo hiyo kubwa ya Shinda Nyumba.
 


Hatimaye Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba iliyokuwa ikiendeshwa kwa zaidi ya miezi 6 na Kampuni ya Global Publishers ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wasomaji wake, imefikia mwisho ambapo mshindi kutoka Dodoma amepatikana.

Katika droo ya fainali hiyo, ambayo imefanyika kwenye Viwanja vya Las Vegas, Mabibo jijini Dar huku mgeni rasmi akiwa Diwani wa Kata ya Mabibo, Kassim Lema, mshindi aliyejishindia nyumba hiyo iliyopo Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar, ni George Majaba mkazi wa Mkoa wa Dodoma.


Akizungumza na Gazeti hili, mapema baada ya kumaliza shughuli ya kumtangaza mshindi wa nyumba hiyo, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho aliwashukuru wasomaji wa Magazeti ya Global kwa kuwa waaminifu katika kipindi chote ambacho wameshiriki kimamilifu kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mshindi. Mbali na mshindi huyo wa nyumba, pia kulikuwa na washindi wengine walioibuka na zawadi za dinner set, ambao ni Kahabi Suleiman wa Vingunguti, Dar, Melania Swai wa Mbezi, Dar na Philemon Faustine wa Dar. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa