Home » » SERIKALI YATAKIWA KULINDA BARABARA ZA LAMI

SERIKALI YATAKIWA KULINDA BARABARA ZA LAMI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu hatua zinazochukuliwa katika ulindaji wa miundombinu ya barabara wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso akitoa maoni kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, juu ya ulindaji wa miundombinu na kuzingatia usalama wa mazingira wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, (watatu kushoto), akiwaonesha kingo za barabara baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakitoka kukagua daraja la Kelema linalounganisha Wilaya ya Chemba na Kondoa, mkoani Dodoma. Daraja hilo limekamilika kwa asilimia 98.


Serikali imetakiwa kuweka mkakati wa kuzilinda, kutunza na kuhifadhi barabara zote zinazojengwa kwa kiwango cha lami nchini ili kuziwezesha kudumu kwa muda uliokusudiwa na hivyo kuepuka gharama za ukarabati wa mara kwa mara.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu mheshimiwa Moshi Suleman Kakoso amesema hayo mara baada ya kukagua barabara ya Dodoma – Babati yenye urefu wa kilomita 263, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika.

“Hakikisheni ujenzi wa barabara unaendana na uboreshaji wa huduma na maisha ya wananchi sehemu ambapo barabara hizo zinapita ili kuchochea maendeleo”, amesema mheshimiwa Kakoso.

Makamu mwenyekiti huyo amesema Kamati yake imeridhishwa na hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara Dodoma –Babati KM na daraja la Kelema linalounganisha Wilaya za Chemba na Kondoa ambalo litawezesha barabara hiyo kupitika kwa uhakika wakati wote.

“Nimefurahishwa na taarifa aliyoitoa Meneja mradi wa barabara hii kwamba pamoja na kujenga barabara pia mkandarasi amechimba visima vya maji katika maeneo haya kwa ajili ya kusaidia wananchi jambo ambalo ni jema na la kuigwa na makandarasi wengine”, amesisitiza Makamu Mwenyekiti Kakoso.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa