Home » » TAASISI ZA FEDHA ZAPEWA SOMO

TAASISI ZA FEDHA ZAPEWA SOMO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TAASISI za fedha nchini zimetakiwa kuboresha huduma zao kwa kuzifanyika kazi changamoto zinazolalamikiwa na baadhi ya wateja wao.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme, wakati alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa benki ya NMB mkoa wa Dodoma.

Mndeme alisema ili taasisi za fedha ziweze kuendelea, zinatakiwa kufanyia kazi changamoto zinazolalamikiwa na wateja wao wenye nia njema ya kuomba kuboreshewa huduma.

“Mimi ni mteja wa benki ya NMB tangu kuanzishwa kwake, lakini kulikuwa na baadhi ya changamoto ambazo zilifanyiwa kazi hadi leo tunaona benki hii imeboresha huduma zake na kuwa kimbilio la wananchi wengi,” alisema.

Hata hivyo, alisema changamoto zinatakiwa kubadilishwa kuwa fursa kwa kuboresha huduma na kuwavutia wateja wao wanaofika katika maeneo hayo, kuweka, kuchukua au kuomba mikopo.

Mmoja wa wateja wa benki hiyo, Juma Mgaza, aliwaomba kuongeza kiwango cha mikopo cha benki hiyo kutoka Sh. milioni 30 hadi Sh.milioni 50.

Meneja wa NMB, Kanda ya Kati, Straton Chilongola, alisema maadhimisho ya wiki ya huduma ya wateja kwa benki huadhimishwa duniani mwezi Oktoba kila mwaka.

Chilongola alisema lengo la maadhimisho hayo ni kujitathmini kuhusu huduma zinazotolewa na benki kwa kukaa na baadhi ya wateja wao ili kupokea changamoto na maoni yao.

Alisema wakati wa maadhimisho, hutoa michango katika jamii hasa ya huduma za afya, shule na vituo vya kutunza wasiojiweza na wenye mazingira magumu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa