Home » » MAMBO YABADILIKA,NABII TITO ASHTAKIWA KWA KUTAKA KUJIUA,MWENYEWE ASEMA ALISIKIA SAUTI IKIMWAMBIA AJIKATE WEMBE.

MAMBO YABADILIKA,NABII TITO ASHTAKIWA KWA KUTAKA KUJIUA,MWENYEWE ASEMA ALISIKIA SAUTI IKIMWAMBIA AJIKATE WEMBE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Onesmo Machibya maarufu ‘Nabii Tito’, mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma mwenye umri wa miaka 45, January 29, 2018 amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Dodoma kwa kosa la kujaribu kujiua.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo James Karayemaha, wakili wa serikali Salome Magesa alisema mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo January 25 2018 huu katika kijiji cha ng’ong’ona.

Alisema ‘Nabii Tito’ alitaka kujiua kwa kutumia wembe ambapo alijijeruhi kwenye baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati akikamatwa na polisi na kwamba ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 217 na kanuni zake.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alipoulizwa na Hakimu alisema alichukua uamuzi huo baada ya kusikia sauti ikisema ajikate na wembe nakudai alitekeleza alichokisikia .

Baada ya kupata maelezo hayo Hakimu huyo alisema kutokana na alichokisikia kutoka kwa Nabii Tito anachukulia kuwa amesema si kweli kuwa ametenda kosa hilo na kuhoji upande wa mashtaka kuhusu upelelezi wa kesi hiyo kama umekamilika.

Hata hivyo kwa mujibu wa kifungu cha sheria 148(5) (b) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 alisema amewasilisha mahakamani kiapo cha kupinga dhamana kwa mshtakiwa chenye sababu saba ambazo hakuziainisha ndani ya Mahakama hiyo.

Kutokana na pingamizi hilo Hakimu Karayemaha alisema mshtakiwa huyo ataendelea kuwa rumande hadi hapo Mahakama itakapoamua kuhusu dhamana yake.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa