Home » » BODI YA AFYA KONDOA MJI YAZINDULIWA

BODI YA AFYA KONDOA MJI YAZINDULIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
  Mkuu wa Wilaya ya Kondoa ( wa tatu kushoto waliosimama) akiwa katika ya pamoja na wajumbe wa bodi ya afya Kondoa Mji  na sekretarieti wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.

 Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota (wa tatu kushoto) akimkabidhi kitendeakazi mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Afya Halmashauri ya Mji Kondoa wakati wa uzinduzi wa wa bodi hiyo hivi karibuni.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mji Kondoa akitoa mafunzo kwa wajumbe wapya wa Bodi ya Afya ya Mji wa Kondoa.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota amewataka wajumbe wa bodi ya Afya Kondoa Mji kutekeleza majikumu yao kwa umakini na weledi ili kuhakikisha kuwa huduma za Afya zinaimarika.
Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bodi ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa jengo la Biashara Kondoa ikiwa ni bodi ya kwanza tangu kugawanywa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na kupatikana kwa Halmashauri ya Mji.
“Kwasasa usimamizi wa Hospitali ya Wilaya utakuwa chini ya Halmashauri ya Mji Kondoa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha hospitali inakua.”alisema Makota
Aliongeza kuwa kwasasa halmashauri haina vituo vya Afya na Zahanati ni chache  hivyo ni jukumu lao kuhakikisha vyote vinaanzishwa na kuongezeka ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato ya Hospitali na zahanati kwa ajili ya kuboresha miundombinu yake.
Aidha akiongea katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mh. Hamza Mafita alisema kuwa wajumbe waliochaguliwa ndio watendaji wakuu wa mabadiliko ya huduma ya Afya hivyo watakutana na changamoto nyingi na wanapaswa kuzitatua na kuzipeleka mbele watakazoshindwa kuzitatua ili washirikiane kuzitatua.
Bodi ya Afya ya Halmashauri ya Mji Kondoa imezinduliwa kwa mara ya kwanza kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo Dkt. Maulid Majala alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi, Emiliana Komolo Makamu Mwenyekiti na Dkt. Eusebi Kessy kuwa Katibu wa Bodi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa