Home » » KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi (katikati) akisisitiza jambo wakati akifungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu lililofanyika tarehe 21Machi, 2018 mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo mjini Dodoma kabla ya kufungua Kikao hicho.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano leo mjini Dodoma kabla ya kufunguliwa kwa Kikao cha baraza hilo .

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi. Maimuna Tarishi ameongoza Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo na kuwaasa wajumbe wa baraza kutoa maoni yatakayosaidia kufanikisha mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2018/2019.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho Tarishi amesema kuwa Watumishi wote katika Ofisi hiyo wanao wajibu wakushiriki kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya bajeti ili kufanikisha azma ya Serikali kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Bila kujali nafasi zenu ni lazima mtambue kuwa mnao wajibu sawa katika kutoa maoni yatakayosaidia katika mchakato wa maandalizi ya bajeti” alisisitiza Bi. Tarishi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa