Na John Banda, Dodoma
Wafanyabiashara ndago ndogo [Machinga] wamekaidi agizo
la Manispaa ya Dodoma la kuwataka wasijenge vibanda katika stendi ya Daladala ya Jamatini
mpaka watakapopewa utaratibu.
Machinga hao waliamua kuanza ujenzi mara tu baada ya
kamati ya Mipango miji kuondoka katika eneo hilo walipofika kukagua na kufanya
uhakiki wa waliokuwepo kabla ya ujenzi wa stendi hiyo kuanza Augost 2012 kama utaratibu ulifuatwa wakati wa ugawaji wa nafasi
za kujenga vibanda katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Machinga hao Haji Kulaya aliwatangazia
wanachama wake kuwa waendelee kujenga vibanda vyao ili waweze kuanza biashara
zao zilizosimama siku nne zilizopita tangu walipohamishwa toka ilipokuwa standi
ya muda ya oil com.
Kulaya alisema wajenge kwa kutumia utaratibu wa
walioutumia viongozi kugawa namba zenye majina ya machinga hao huku wakiuka
agizo la Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji Stephen Mwanga aliyewataka
kutofanya chochote mpaka watakapopewa maelekezo toka manispaa.
Kamati hiyo ilifika katika stendi hiyo na kutokana na
kupokea malalamiko toka miongoni mwa machinga hao ambao hawakuwa wamelidhika
kutokana na kuwatuhumu viongozi wao kugawa nafasi kwa upendeleo huku
wakiwaingiza watu ambao hawakuwepo awali katika stand hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira
manispaa Stephen Mwanga alikaliliwa kuwa
walifika na kuamua kufanya uhakiki kwa wafanyabiashara hao na jumla yao ni 88
tofauti naya viongozi wao waliokuwa na 122 huku wageni hasa wanawake wakipewa
kipaumbele.
“Tuliamua kufanya uhakiki ule kwa kutumia watu halisi
waliokuwepo kwamaana walijuana kila mtu na jirani yake, tuligundua mama lishe
14, wenye vibanda 69, ugogo na upendo Group 7 jumla 88, huku waliokuwa na
mezana,mboga mboga na matunda watafanyiwa utaratibu maarumu ili kuondoa malalamiko”,
alisema Mwanga
Aidha aliongeza kuwa wao kama manispaa wenye stend na
watu walifika ili kuondoa kelo na malalamiko yaliyokuwepo lakini kama watajenga
bila mikataba wajiandae kuondolewa na wasimulaumu mtu nguvu ya Dola
itakapotumika.
Kwa upande wake Naibu Meya manispaa ya Dodoma Jumanne
Ngede alisema kutokana na ujenzi wa stendi hiyo kugharim Mabilion ya Fedha
wamepanga vibanda vyote vitakavyowekwa katika stend hiyo kuwa na paa moja,
Rangi Moja na viwekwe kwenye mcholo.
Ngede aliongeza kuwa watahakikisha kila mtu atakaepata
nafasi katika stendi hiyo wataingia nae mkataba na kutokana na orodha waliyo
nayo itakuwa rahisi kujua machinga hao wataiingizia Halimashauri pato kiasi
gani katika makusanyo.
“Tumejenga Stendi ya Kisasa na kutokana na kuwa huu ni
mji wa makao makuu lazima kama inavyo ng’a hivi ndivyo iendelee Kung’aa hata na
kwa wenye vibanda ili waendane nayo, na kutokana na mkataba hatutasumbuana na
mtu juu ya ukusanyaji wa mapato”, alisema Ngede.
0 comments:
Post a Comment