Home » » BALOZI WA CHINA AAHIDI KUCHIMBA KISIMA DODOMA

BALOZI WA CHINA AAHIDI KUCHIMBA KISIMA DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge ambapo aliahidi kutoa msaada wa kuchimba kisima kimoja cha maji Mkoani Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na Balozi wa China Mheshimiwa Wang Ke (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo yao, kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge na kulia ni Afisa kutoka Ubalozi wa China.

Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Makao Makuu

Balozi wa China hapa nchini Mhe.Wang Ke ameahidi Serikali yake itatoa msaada wa kugharamia mradi wa uchimbaji kisima kimoja cha maji na miundombinu ya usambazaji wa huduma hiyo kwenye moja ya kijiji cha Mkoa wa Dodoma.

Balozi Wang Ke alimuahidi msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge leo alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma, ambapo alimtaka Dkt. Mahenge kutumia timu ya Watalaalamu wa Maji wa Mkoa kufanya usanifu na makadirio ya bajeti ya mradi huo na kuiwasilisha Ofisi za Ubalozi wa China kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi.Aidha, Balozi Wang Ke ameelezea kuwa Uongozi wa Mkoa utaainisha ni kijiji kipi ambacho kitapewa fursa ya kupatiwa mradi huo.

Kwa upande wake, Dk. Mahenge ameishukuru Serikali ya China kupitia kwa Balozi Wang Ke kwa ajili ya mradi huo na amebainisha kuwa mradi huo pia unaweza ukatumika kuwasaidia vijana kwenye kijiji kitachopewa mradi kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Dkt. Mahenge amemwelezea Balozi Wang Ke kuwa amefanya ziara kwenye Wilaya za Mkoa wa Dodoma na amejionea namna ambavyo wananchi wanahitaji kubwa la maji na hivyo mradi huo umekuja wakati muafaka kabisa.

Katika mazungumzo ya Viongozi hao, mradi huo utahusisha Utafiti wa uwezekano wa kupata maji chini ya Ardhi, Uchimbaji wa Kisima kirefu, ununuzi wa mashine ya kuvuta na kusukumia maji, ujenzi wa Miundombinu ya kusambazia maji, Tenki la kuhifadhia maji na vituo vya wananchi kuchotea maji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa