Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe. Almasi Athuman Maige (Mb), akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichokutana kumhoji Mhe. Saed Kubenea (Mb) kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea alifika mbele ya Kamati hiyo leo ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano yake yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea (Mb) akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea amefika mbele ya Kamati hiyo leo kwa mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano hayo yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.PICHA NA BUNGE
Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji Mbunge wa Ubungo
Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.
Akizungumza
mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mheshimiwa Almasi Athuman Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa Kubenea
amefikishwa mbele ya Kamati hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na
kauli aliyotoa kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34
(1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mheshimiwa
Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika leo baada ya kuahirishwa mara
mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya
na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe.
Mheshimiwa
Maige aliongeza kuwa baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa
Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai
kwa hatua zaidi.
“Kanuni
zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia
kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa
Bungeni,” alisema.
0 comments:
Post a Comment