Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Aweso
Mbali
na hayo, Mhe. Aweso ameshauri Halmashauri za Manispaa katika Jiji la
Dar es Salaam kutunga na kusimamia Sheria ndogo kwa ajili ya kudhibiti
uchafuzi wa maji ya mito hiyo.
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO, DODOMA
Serikali
itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kufanya shughuli za
kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga katika maeneo sahihi.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Aweso wakati
akijibu swali la Mhe. Zainabu Amiri kuhusu Mpango wa Serikali wa
kuwapatia maji safi na salama wakulima hao wa mbogamboga.
Mhe.
Aweso amesema kuwa Wizara ya Maji kwa kuzingatia umuhimu wa afya za
wananchi inaendelea kutoa miongozo na ushauri kuhusu maji yanayofaa kwa
matumizi ya binadamu na kwa shughuli za uchumi.
"
Katika kuhakikisha wananchi wanalima mbogamboga katika maeneo sahihi,
Serikali iliunda kikosi kazi kwa kushirikisha maafisa wa Baraza la
Mazingira la Taifa(NEMC) ambapo kilitembelea baadhi ya mito ya Dar es
salaam na kugundua uchafuzi mkubwa wa mazingira unaosababishwa na
utiririshaji wa majitaka kutoka majumbani na kwenye viwanda ambapo maji
hayo kuwa na kemikali zisizofaa kwa matumizi ya kilimo cha mbogamboga
kwa mfano mto Msimbazi" amesema Mhe. Aweso.
Aidha,
Naibu Waziri huyo amesema kuwa, Serikali inawataka wananchi kuacha
kulima mbogamboga katika maeneo hayo yenye uchafuzi kwa kuwa maji hayo
yana athari kwa afya.Vilevile
amesema kuwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira) inaendelea kupima maji ya mito hiyo na kutoa
taarifa za hali ya maji hayo.
0 comments:
Post a Comment