Home » » WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MVUA KWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MVUA KWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Serikali imewataka Viongozi na wananchi wote kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu leo Mjini Dodoma, wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu tahadhari kwa umma kuhusu mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Mhe. Ikupa amesema kuwa, mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania ilitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba mpaka Desemba 2017 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua.

Aidha, ameongeza kuwa kutokana na taarifa hiyo serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ilielekeza Wizara na mamlaka za Serikali za Mitaa kuchukua hatua stahiki kwa kutumia mvua hizo kwa shughuli za uzalishaji mali pamoja na na kuchukua hatua za tahadhari kwa madhara yanayoweza kujitokeza.

“Kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya kijiji na mitaa zinatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017 ya kuchukua hatua za kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa kukabiliana na maafa endapo yatatokea,” amesema Mhe. Ikupa.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa