Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya maafisa wa TASAF wakitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la maonyesho la TASAF kwenye viwanja vya nane nane ,Nzuguni nje kidogo ya mji wa Doodoma.
Mmoja wa walengwa wa TASAF kutoka kikundi cha Wakulima wa Mwani Msichoke cha Bagamoyo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TASAF. Kikundi hicho kimewezeshwa na TASAF na sasa kinatengeza sabuni na mafuta kutokana na zao la mwani kama njia ya kujiongezea kipato.
Mtaalam wa Mawasiliano wa TASAF Bi. Zuhura Mdungi akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la maonyesho la TASAF lililoko kwenye jingo la Ofisi ya Rais kwenye eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Mmoja wa maafisa wa TASAF, Bi. Grace Kibonde akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la TASAF kwenye maonyesho ya nane nane kwenye eneo la Nzuguni nje kidogo ya mjini Dodoma.
Na Estom Sanga-TASAF
Vikundi
vya baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini
unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kutoka mikoa ya
Dodoma, Pwani Manyara na Singida vinashiriki kwenye maonyesho ya nane
nane yaliyoanza mwanzoni mwa wiki hii mjini Dodoma.
Vikundi
hivyo vilivyoko kwenye banda la Ofisi ya Rais kwenye eneo la maonyesho
la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma, vinaonyesha bidhaa
zilizotengenezwa na vikundi hivyo baada ya kuwezeshwa na TASAF ikiwa ni
njia mojawapo ya kuinua shughuli za uzalishaji mali na kuongeza mapato
ya walengwa wa Mpango huo wenye lengo la kusaidia jitihada za serikali
za kuwapunguzia wananchi kero ya umasikini.
Bidhaa
zinazotengenezwa na vikundi hivyo na ambazo zimeletwa kwenye maonyesho
hayo ni pamoja na sabuni na mafuta ya manukato ambavyo vimetengenezwa
kwa kutumia mmea wa mwani ambao humea kwenye maeneo ya baharini.
Bidhaa
nyingine ambazo zimezalishwa na vikundi hivyo vya walengwa wa TASAF ni
pamoja na asali,ubuyu,mafuta ya alizeti na mifuko bora ya kuhifadhia
nafaka ambavyo vimetokana na kazi za mikono ya walengwa hao ikiwa ni
maojawapo ya sharti la kuzifanya kuinua uchumi na kujiongezea kipato kwa
njia ya vikundi.
Walengwa
hao wamepongeza hatua ya serikali kupitia TASAF kuwashirikisha kwenye
maonyesho hayo kwani hatua hiyo inasaidia kutangaza shughuli za
uzalishaji mali zinzofanywa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya
masikini ambao wanahitaji masoko ya bidhaa wanazozizalisha ili kukuza
uchumi wao.
0 comments:
Post a Comment