WIZARA YA FEDHA, TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZABADILISHANA UZOEFU WA DAFTARI LA KIELEKTRONIKI LA TAARIFA ZA MAAFISA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI

Na Martha Mbena na Jordan Mbwambo, WF, Dodoma

Watumishi wa Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma na wa Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar, Idara ya Usimamizi Sera za Umma, wamebadilishana uzoefu kuhusu matumizi ya Daftari la Kielektroniki la Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi Serikalini.

Watumishi hao wamekutana jijini Dodoma kwa ajili ya kujifunza namna ya usanifu na ujenzi wa  Daftari la Kielektroniki la Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi Serikalini (Procurement and Supplies Personnel Information System – PSPIS) ambalo hutumika kama zana ya utekelezaji wa matakwa ya Kifungu  cha  7(j) cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya Mwaka 2023, kinachoipa Wizara jukumu la kushauri kuhusu muundo, uteuzi wa Wakuu wa Vitengo vya Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi, na kupendekeza uhamisho wa watumishi wa ununuzi na ugavi.

Akizungumza wakati wa kikao kazi hicho, Kaimu Kamishna wa Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bw. Alex Haraba, amesema kuwa Mfumo wa PSPIS ni nyenzo muhimu inayosaidia Serikali kuwa na taarifa sahihi za watumishi wanaotekeleza majukumu ya ununuzi wa umma na ugavi.

“Matumizi ya Mfumo huo yanawezesha taarifa za maafisa wa ununuzi na ugavi kukusanywa na kusimamiwa kwa ufanisi, hatua inayosaidia Serikali kufanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa sahihi na zinazopatikana kwa wakati,” amesema Bw. Haraba.

Amesema taarifa hizo ni muhimu katika kupanga rasilimali watu, kutambua mahitaji ya kada, kujenga uwezo wa watumishi na kutoa ushauri wa kisera na kiutendaji.

Aidha, daftari la watumishi wanaofanya kazi za ununuzi na ugavi katika Vitengo vya Usimamizi wa Ununuzi (PMUs) ni nyenzo ya kiutawala inayolenga kuiwezesha Serikali kuwa na kumbukumbu sahihi, zilizohakikiwa na zinazosasishwa kuhusu watumishi hao.

Pia, katika kikao kazi hicho, wataalamu wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Kifedha na huduma za ndani, Wizara ya Fedha, walitoa maelezo kuhusu matumizi ya Mfumo wa PSPIS na namna ulivyounganishwa na Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) kama mbinu ya kuhakikisha mifumo hii inabadilishana taarifa kwa usahihi.


Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bw. Alex Haraba, akiagana na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi Zanzibar, Bi. Asma Mohamed, baada ya kukamilika kwa mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma. 
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Mali za Umma, Bi. Emma Komba, akiagana na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi Zanzibar, Bi. Asma Mohamed, baada ya kukamilika kwa mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma
Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Mali za Umma, Bw. Alex Haraba, akichangia hoja wakati wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi Zanzibar, Bi. Asma Mohamed, akichangia hoja wakati wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Wandamizi kutoka Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma Tanzania Bara, wakifuatilia mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.

Maafisa Ugavi Wandamizi kutoka Wizara za Fedha za Tanzania Bara na Zanzibar, wakifuatilia kwa umakini mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi, yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bw. Amir Mlenge, akichangia hoja wakati wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi, yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bw. Richard Benaya, akichangia hoja wakati wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi, yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.

Watumishi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma kutoka Wizara za Fedha za Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilika kwa mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Maafisa Ununuzi na Ugavi, yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.

(Picha na Kurugenzi ya Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha)


MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagwa rasmi na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini yake katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. 

Jumatano Septemba 09, 2026 Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughukia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Menejimenti ya Wizara na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewaasa Viongozi na Watendaji hao kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Wasaidizi wake ili waendelee kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia Watanzania. 

 Aidha, Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uzalendo ili kutimiza matarajio ya wananchi kwa Serikali.










WATU WANNE WAFARIKI BAADA YA BASI LA ABOOD KUGONGA TOYOTA IST BUNJU

Watu wanne wamefariki dunia baada ya basi la kampuni ya Abood kugongana na gari dogo aina ya Toyota IST katika eneo la Bunju Sokoni, Barabara ya Bagamoyo, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, ajali hiyo ilitokea Septemba 7, 2026, majira ya saa 1:40 usiku.

 Basi lenye namba za usajili T 235 EMJ, aina ya Yutong, liligongana na gari lenye namba T 274 ERU, aina ya Toyota IST.

 Basi hilo lilikuwa likitokea Tegeta kuelekea Bunju, likiwa na safari ya kwenda mkoani Tanga. Lilikuwa likiendeshwa na Christivian Steven Shemuhilu, mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Kange, Tanga.



 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa