TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imekabidhi rasmi

 eneo la mradi kwa mkandarasi TIL Construction Limited kwa ajili 

ya kuanza ujenzi wa jengo jipya la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu

 (STI)  jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kukabidhi eneo hilo la mradi 

Machi 25,2025 jijini Dodoma  Mratibu Msaidizi wa Mradi

 wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) 

kutoka COSTECH, Dkt. Aloyce Andrew, amesema hatua hiyo

 inalenga kurahisisha utoaji wa huduma kwa wadau wa taasisi hiyo.