Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza na Waandishi wa Habari Mijini Dodoma (Hawapo Pichani) akitoa
tamko la Wizara juu ya ugonjwa wa homa ya Zika kushoto ni Mganga Mkuu
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula. Picha Na
Raymond Mushumbusi Maelezo
Na Raymond Mushumbusi Maelezo
Wananchi wa Tanzania watahadharishwa juu ya ugojwa wa homa ya Zika uliripotiwa kutokea katika nchi za Amerika ya kusini hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mijini
Dodoma na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy
Mwalimu alipokuwa akitoa tamko juu ya uvumi ulioenea kuhusu homa ya
Zika iliyoenea katika nchi za Amerika ya kusini.
Mhe.Ummy Mwalimu amewaasa watanznia kuwa na tabia ya kwenda hospitali
kila wanapojisikia dalili za homa na kupima kwani sio kila homa ni
malaria kwani dalili za homa ya malaria zinafanana kabisa na dalili za
ugonjwa wa homa ya Zika.
“ Nawaomba ndugu zangu watanzania tuzingatie usafi ili kuzuia mazalia ya
mbu kwani ugonjwa huu unatokana na virusi vinavyoenezwa na mbu na hao
mbu wanapatikana sana nyakati za asubuhi mchana na jioni hivyo nawasihi
kutumia dawa za kuua mbua na vyandarua wakati wa kulala.”
“Napenda kutoa tamko kuwa ugonjwa huu wa homa ya Zika haujaingia
Tanzania na tunawaomba watanzania kuwa makini sana na waripoti dalili
zozote ambazo sio za kawaida zitakazojitokeza na mpaka jana kwa taarifa
tulizonazo hakuna mgonjwa aliyegundulika kuwa na homa ya Zika” Alisema Mhe.Mwalimu.
Aidha naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu
Chaula amesema wamejiandaa kukabiliana na kesi zozote zinatazojitokeza
za homa ya Zika na wana mfumo mzuri wa kubaini magonjwa ya mlipuko na pia kuna maabara ya NIMR ambayo inafanya uchunguzi juu ya magonjwa mbalimbali.
“ Nawaomba watanzania kutopuuzia dalili zozote za homa na kuamua
kujitibia manyumbani au kunywa dawa bila kupima na kujua hiyo homa ni
ugonjwa gani kwani yaweza kuwa homa ya Zika” Alisema Dkt Chaula.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee wa kushirikiana na
Shirika la Afya Dunianoi (WHO) wanafatilia kuhusu ugonjwa huu na watatoa
maelekezo ya kuzingatia ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu ila mpaka
sasa ugomjwa huu haujaingia Tanzania.
0 comments:
Post a Comment