Home » » BUNGE LA KATIBA LATUMIA SH.BILIONI 27

BUNGE LA KATIBA LATUMIA SH.BILIONI 27

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Kastiba,Saada Mkuya,akichangia katika bunge hilo mjini Dododoma jana.
Hadi  kufikia jana serikali imetumia Sh. bilioni 27 kuendesha Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha ambaye pia ni mjumbe wa bunge hilo, Saada Mkuya Salim, aliliambia Bunge Maalumu jana.

Aliwaeleza wajumbe kuwa serikali imesitisha hata kupeleke maji, umeme na huduma nyingine muhimu vijijini ili kuwezesha kuandikwa katiba hiyo.

Kadhalika imejitahidi  kila wakati kuwapa wabunge stahili zao na mara nyingi wajumbe hawajacheleweshewa kupata hela zao.

Aliongeza kuwa lengo ni kutaka bunge lifanikiwe kwa sababu taifa linataka wakiondoka kipatikane kitu chenye maana.
 
AWAANGUKIA UKAWA
Akiwazungumzia wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) waliosusia bunge hilo tangu Jumatano iliyopita alisema anasikitishwa na baadhi ya wajumbe kususia majadiliano hayo.

 Alisema kuna changamoto nyingi zinazoikumba nchini na fursa ya kuandika katiba ndiyo inayostahili kutumika kuzipatia ufumbuzi.

“Kote kuna changamoto upande wa Tanzania Bara na Zanzibar zipo kwenye kutekeleza katiba na pia sheria.Lakini hazitatuliwi kwenye mikutano ya Kibanda Maiti ni hapa ndani ya ukumbi wa bunge maalumu,” alisema  na kuwataka wajumbe wa Ukawa  warejee mkutanoni.

“Mkutano huu jamani  ni kama umekwenda kwenye majadiliano usitegemee kupata kila unachokitaka itabidi wakati mwingine ukubaliane na wenzako. Japo si wakati wote kwani unaweza kupata kile ulichokikusudia,” aliwasihi wajumbe hao.

Aliongeza kuwa kutoka nje na kufanya katiba nyingine  nje  ya ukumbi hakulisaidii taifa.

“Kwa ajili ya kuwahurumia wananchi wetu walipa kodi wa nchi hii tutumieni  fursa hii tuandike katiba na pia tujali fedha ya wananchi,” alisema Mkuya,
 
SERIKALI TATU
Aliendeleza wimbo kuwa muundo huo wa serikali utaongeza gharama za uendeshaji kwa vile  kila mwaka bajeti ya serikali haitoshi kuendesha hata hizi serikali mbili.

Alisema mapato ya taifa hayajaweza kukidhi haja za mahitaji moja na kila wakati anapokea simu kutoka wilayani zikiulizia fedha za maendeleo ambazo pia ni kidogo.

Alisema Watanzania wanalalamikia kuongezeka kwa matumizi ya serikali kunakoletwa na kuongeza  mikoa na  wilaya itakuwaje kwa kuongeza serikali ya tatu?

Aliwataka wajumbe waangalie suala la kutatua matatizo ya Muungano kwa kuongeza serikali nyingine kwani ni kitu kinacholeta hali ya ‘kusadikika’ zaidi kuliko uhalisia.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa